Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi, Jehad A. Jehad (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu semina ya 26 siku moja itakayo washirikisha wadau wa Sekta ya ujenzi itakayofanyika kesho kutwa Septemba 22, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa.
Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Utawala, Angelo Ngalla, Mwanasheria, Ibrahim Mohamed na Ofisa Uhusiano, Hamisi Sungura.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.Na Dotto Mwaibale
BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi kesho kutwa inatarajia kuendesha semina ya siku moja kwa ajili ya kuwanoa wadau wa sekta ya ujenzi nchini.
Hayo yamebainishwa na Msajili wa Bodi hiyo, Jehad Jehad wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu semina hiyo muhimu itakayofanyika kesho kutwa ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
"Semina hii ambayo ni ya 26 ni muhimu sana kwetu sisi watu wa sekta ya ujenzi hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linatutegema" alisema Jehad.
Alisema semina ya namna hiyo zilianzishwa tangu mwaka 2003 na hufanyika mara mbili kwa mwaka ambapo jumla ya wabunifu majengo, wakadariaji majenzi na wadau wengine wa sekta ya ujenzi wapatao 5,328 wamekuwa wakinufaika na semina hizo.
Alisema malengo ya semina hiyo ni kuwanoa wabunifu majengo na wakadariaji majenzi na wadau wengine katika sekta ya ujenzi kutambua fursa ambazo ziko katika soko la Afrika Mashariki (EAC) na lile la Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)
Alitaja lengo jingine kuwa ni kuwafahanisha wadau faida na umuhimu wa sheria ya mtandao katika kuboresha huduma zao kwa wananchi na kubadilishana uzoefu wa kazi zao za kitaaluma kwa lengo la kuongeza weredi pamoja na kuwapa fursa waataamu katika sekta ya ujenzi kupata nasaha kutoka kwa viongozi wa Serikali.
Jihad aliswema katika semina hiyo mada mbalimbali zitatolewa na kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
0 comments:
Post a Comment