Kwenye harambe hiyo iliyoudhuriwa pia na waziri wa viwanda na biashara mheshimiwa Charles Mwijage jumla ya pesa zilizochangwa ni shilingi za kitanzania 1,396,000,000/=.
Pesa hizo taslimu na ahadi zilizotolewa na wageni mbalimbali waalikwa. Ambapo zimetolewa katika mafungu yafuatayo milioni 700, milioni 600, Euro 10,000 na Dola 10,000 na kufanya jumla yake kuwa 1,396,000,000/= kwa pesa za Tanzania.
Pia wafanyabiashara wakubwa wa makampuni matatu tofauti wameungana na kuahidi kukamilisha ukarabati wa shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ndani ya siku thelathini kuanzia leo, makampuni hayo ni Oil Com, GPP na Moyo Group.
Baadhi ya wafanyabiashara waliochangia michango yao ni pamoja na Regnald Mengi (Milioni 110), umoja wa wauza mafuta ya rejereja (Milioni 250), Kiwanda cha sukari Kagera (Milioni 100), IPTL (Milioni 100), China (Milioni 100) Dewji Foundation (Milioni 100), Mambo ya Nje (Milioni 10), Azania (Milioni 20).
Jumla ya fedha na ahadi zilizotolewa kuwasaidia waathirika tetemeko la ardhi ni takribani Sh1.4 bilioni pamoja na vifaa vya ujenzi
Tetemeko hilo lililotekea Septemba 10,2016.
0 comments:
Post a Comment