Na
Ally Daud-Maelezo.
MAUZO katika Soko la
Hisa Dar es salaam (DSE) yameshuka kwa asilimia 81 kutoka Tsh. Bilioni 9 mpaka
kufikia shilingi bilioni 1.7 kutokana na kushuka kwa idadi ya uuzaji wa hisa
kufikia shilingi 340,000 kwa wiki hii.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Afisa Mwandamizi wa masoko wa DSE
Bi. Mary Kinabo amesema kuwa mauzo hayo yameshuka kutokana na ukubwa wa mtaji
wa soko kushuka kwa asilimia 2.79 kutoka trilioni 21.3 kufikia trilioni 20.7.
Aidha Bi. Mary amesema kuwa ukubwa wa mtaji kutoka
makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha shilingi trilioni 8.2
kutoka wiki iliyopita.
Bi. Mary amesema kuwa
licha ya idadi ya mauzo kushuka pia
Benki ya CRDB imeshika nafasi ya kwanza katika kuuza na kununua hisa kwa
asilimia 53 ikifuatiwa na kampuni ya Bia nchini TBL kwa asilimia 35 huku kampuni
ya Swissport ikishika nafasi ya tatu ya kununua hisa kwa asilimia 3.
Mbali na hayo Bi.
Mary amesema kuwa licha ya viashiria vya soko kushuka kwa alama 36.6 baada ya
bei za hisa kutoka TBL kushuka kwa silimia 1.08, viashiria vya huduma za kibenki na kifedha
vimepanda kwa alama 3.64 baada ya mauzo ya DSE kupanda kwa asilimia 11.5.
0 comments:
Post a Comment