Na Godfriend Mbuya
Msanii wa Bongo Flava Dudu Baya amesema mwanaharakati halisi
hawi na kitambi hivyo watu wanaosema kwamba kapungua siyo wakweli kwa kuwa yeye
kazi zake ni za kiharakati.
Dudubaya ameyasema hayo katika kipindi cha FNL kinachorushwa
na EATV ambapo amewatolea mifano Muasisi wa haki sawa Afrika Kusini Nelson
Mandela pamoja na Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere.
“Mwanaharakati siku zote hawi na kitambi, angalia
mwanaharakati na Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini na Rais wa kwanza wa
Tanzania Baba wa Taifa Mwl. J.K Nyerere hawakuwa na vitambi kutokana na kazi
waliyokuwa wanaifanya” Amesema Dudu Baya.
0 comments:
Post a Comment