Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Tarehe: 21/09/2016
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
amewapongeza Wachezaji wa Kilimanjaro Queens kwa niaba ya serikali na
kwa niaba ya watanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka kuwa mabingwa
wa kwanza wa Kombe la CECAFA kwa mpira wa miguu kwa wanawake Afrika
Mashariki na Kati.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Nnauye alipokua akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
“Kama
serikali ni vyema kuipongeza timu yetu ya Kilimanjaro Queens kwa
kuiwakilisha vizuri Tanzania katika michuano CECAFA na kuibuka mabingwa
kwa kuweza kuruka vizingiti vyote vilivyokuwepo katika muchuano hiyo”
alisema Mhe. Nnauye
Serikali
itaendelea kuweka nguvu ya kutosha na kuungana na timu zetu kuwasaidia
kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika michezo mbalimbali, amesema
Mhe. Nnauye.
Mhe.
Nnauye amesema kuwa Tanzania inaanza kuona matunda ya uwekezaji wa muda
mrefu kwani haikuwa kazi raisi kwa Kilimanjaro Queens kufikia fainali
na kuwa mabingwa kwa kupambana na timu ngumu na kuweza kushinda.
Aidha
Mhe. Nnauye amewahaidi wachezaji wa Kirimanjaro Queens kuwaalika
bungeni katika Bunge lijalo kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaandalia
mechi ya kirafiki kutambua mchango wao wa kuipeperusha bendera ya
Tanzania kati yao na wabunge wanawake.
Timu
zilizoshiriki katika michuano ya kombe la chalenji la CECAFA ni pamoja
na Tanzania, Burundi, Zanzibar, Kenya, Ethiopia, Rwanda pamoja na
mwenyeji Uganda. Mashindano ya Kombe la Chalenji la CECAFA kwa timu za
wanawake yamefanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa
michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa nchi za
Afrika Mashariki na Kati.
0 comments:
Post a Comment