Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dar es Salaam
8.9.2016
RAIS John Pombe Magufuli amewataka
Viongozi na wananchi wa Sudan Kusini kutanguliza mbele maslahi ya nchi
yao ili kusaidia kumaliza mgogoro wa kisiasa unaondelea nchini humo.
Akizungumza
katika mkutano wa 17 wa Jumuiya hiyo leo Jijini Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli alisema jumuiya hiyo inasikitishwa na mapigano
ya ghafla yaliyoibuka hivi karibuni nchini humo.
Rais
Magufuli suala la amani na usalama ni jambo umuhimu si kwa ustawi wa
maendeleo ya taifa hilo pekee bali pia kwa mustakabali wa mataifa
mengine yaliyopo ndani ya jumuiya hiyo.
Aidha
Rais Magufuli aliipongeza Jumuiya ya Ushirikiano wa Kieneo ya Mashariki
mwa Afrika (IGAD) inayoundwa na nchi za Eritrea, Kenya, Somalia, Sudan
Kusini, Sudan na Uganda katika jitihada zake kusuruhisha mgogoro huo.
Aidha
Rais aliipongeza nchi ya Sudan Kusini kuwa mwanachama kamili wa Jumuiya
hiyo na kuwahakikishia kuwa jumuiya hiyo itatoa ushirikiano wa kutosha
katika kuhakikisha ikuwa nchi inapata amani ya kudumu ili wananchi wake
washiriki katika shughuli za maendeleo.
“Sekretarieti
ya jumuiya hiyo inaendelea na maandalizi ya kujumuisha nchi ya Sudan
Kusini katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na nchi
wanachama” alisema Rais Magufuli.
Kwa
upande wake, mwakilishi maalum wa Rais wa Sudan Kusini, Aggrey Tisa
Sabuni aliishukuru jumuiya hiyo kwa uamuzi wa kuikubali nchi hiyo kuwa
mwanachama mpya wa jumuiya hiyo na kuwakikishia kuwa taifa hilo
litarejeshea hali ya utulivu na usalama.
“Jaribio
la mapinduzi la mwezi julai mwaka huu limeleta athari kubwa kwa
wananchi wetu, hata hivyo tunawahakikishia kuwa tutakuwa mshirika wa
kweli wa jumuiya hii” alisema Sabuni.
0 comments:
Post a Comment