Na Sheila Simba-MAELEZO
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka
wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuiwezesha nchi
kufikia uchumi wa kati kupitia ujezi na uendelezaji viwanda.
Amesema
hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa 14 wa Bodi ya Wahandisi
Nchini,na kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia uchumi wa
kati ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.
“mkiamua
nchi iende kwenye uchumi wa kati inawezekana lakini kama mtaamua
isiendi pia inawezekana hivyo basi uzalendo unahitajika katika kufanya
kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema Rais Magufuli.
Aidha
amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi
miongoni mwao hasa kwenye utendaji kazi na miradi ya maendeleo.
“Tumemsikia
waziri akisema serikali inamapango wa kukarabati na kununua meli mbili,
wahandisi jiulizeni mmejipangaje kutumia fursa hii kwa kuomba tenda na
naamini serikali haiwezi kukataa ombi hasa kwa wahandisi wa
ndani”Alisema Rais Magufuli
Akimkaribisha
rais Magufuli katika mkutano huo waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Prof Makame Mbarawa alisema kuwa licha sekta ya miundo mbinu
kufanya vizuri hasa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,Serikali
itaendelea kulipa kipaumbele ujenzi wa barabara kuanzia
viijiji,Halmashauri na za mikoa.
“serikali
inafanya jitahada kujenga miondo mbinu imara ili kurahisisha usafiri wa
kutoka sehemu moja kwenda nyinfine na ukarabati wa kiwanja cha ndege
cha Dodoma umekamilika kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu
Lema amemuomba Rais kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki katika
miradi mikubwa ili kujifunza kupitia miradi hiyo.
Aidha
Mhandisi Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi
milioni 100 kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa
shule za sekondari nchini.
akizungumza
katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda
alitangza tarehe mosi oktoba kuwa siku ya kupanda miti katika mkoa wa
Dae Es Salaam.

0 comments:
Post a Comment