Serikali kupitia
Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi limesema kuwa litaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kutatua changamoto ya
ajira kwa vijana.
Hayo yamesemwa juzi
Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Vijana katika Ofisi ya Waziri Mkuu, James Kajugusi wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya ujasiriamali
kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu nchini.
“Uwezeshaji wananchi
kiuchumi ni dhana pana inayohitaji ushirikiano wa karibu kati ya serikali na
sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo na katika kuchochea juhudi za
uwezeshaji wananchi kiuchumi” alisemaBw.Kajugusi
Akizungumzia kuhusu changamoto
zinazowakabili vijana nchini, Kajugusi alisema kuwa changamoto ya ukosefu wa
ajira kwa vijana imechochewa na mabadiliko ya kisera na kiuchumi yanayosimamiwa
kwa dhati na serikali katika kupeleka mbele zaidi taifa letu katika nyanja za
kijamii na kiuchumi.
Awali akizungumza na
vijana 22 waliohitimu mafunzo hayo aliwataka vijana hao kuongeza ari ya kufanya
kazi na kushiriki fursa mbalimbali
zinazojitokeza zenye lengo la kujikwamua kiuchumi.
“Vijana mtumie vema
fursa mbalimbali za uwezeshaji mnazozipata kwa kuboresha zaidi uelewa wenu na hali zenu za maisha” Alisema
Kajugusi
Kwa upande wake Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi, Bi Anna Mtaita amesema kuwa Baraza hilo
litaendelea kuthamini nchini na kwa
kulitambua hilo maana wameamua kushirikiana na taasisi ya maendeleo ya
Cambridge katika kuratibu na kutoa mafunzo hayo.
Mtaita aliongeza kuwa
mbali na programu hiyo, Baraza hilo pia linaratibu programu ya majaribio kwa
vijana walio katika mazingira magumu katika kuwapatia mafunzo, malezi, na
kuwaunganisha na mitaji.
Kwa mujibu wa Mtaita
alisema mpaka kufikia sasa Baraza hilo limewawezesha vijana 500 nchini katika
upataji wa mafunzo, malezi na mitaji.
0 comments:
Post a Comment