Na Mwandishi wetu
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kushikilia msimamo wake wa kupinga ndoa za jinsia moja,kuongeza uwigo wa uhalalishaji wa
utoaji mimba,adhabu ya kifo,kuweka sera ya kutonyonga wanaokutwa na
adhabu ya kifo na uridhiwaji wa mikataba ya Kimataifa inayozuia masuala
ya utesaji kwa kuwa masuala hayo yanaonekana kutoendana na Katiba na
Sheria za nchi, Sera,mila desturi na tamaduni za watanzania ikiwa ni sehemu ya mapendekezo 72 yaliyokataliwa na Serikali wakati wa mapitio ya taarifa ya nchi ya ukuzaji na usimamizi wa haki za binadamu.
Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu Gerson Mdemu ameyasema hayoleo
jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga kikao maalumu cha siku mbili cha
wadau mbalimbali wa masuala ya haki za binadamu ambapo ameeleza kuwa Serikali ilipokea jumla ya mapendekezo 227 yaliyotolewa
na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi Mei 2016 chini
ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum (The Universal Periodic Review).
Mdemu ameongeza kuwa mapendekezo hayo kwa ujumla yalijikita katika majukumu
ya Tanzania kwenye mikataba ya kimataifa ,Mifumo ya kikatiba na
kisheria,miundombinu ya kitaasisi ya haki za binadamu ,masula ya
kisera,ushirikiano na vyombo vya kikanda na kimataifa,utawala wa
sheria,uendeshaji haki,masuala ya kulinda haki za msingi za binadamu
kama vile haki ya kuishi,haki ya afya,haki za walemavu,watoto,haki ya
habari na kujieleza,afya elimu mazingira haki za watu asilia na
wakimbizi.
Hata hivyo, Tanzania ilikubali kutekeleza mapendekezo 130 tu kati ya 227 yaliyokuwa yanahusu
mchakato wa Katiba,kuijengea uwezo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora, kuhuisha Sera za nchi ili ziendane na malengo endelevu ya Dunia
,kuandaa taarifa za nchi za utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu
na kuziwasilisha kwenye vyombo vya vya umoja wa mataifa kwa wakati.
Vilevile Serikali iliahirisha jumla ya mapendekezo 25 ambayo yalijikita katika marekebisho
ya sheria ya Takwimu, 2015, Sheria ya makosa ya mtandao,
2015,ukamilishaji wa Sheria ya Habari, Sheria ya vyombo vya
Habari,uandaaji wa mikakati na mipangokazi ya utekelezaji wa msuala ya
kuzuia ndoa za utotoni na za kulazimishwa ,upitishaji wa sera mpya
mbalimbali ikiwemo ya kutoa vyeti vya kuzaliwa na usajili wake kuwa bure
na masuala ya uchaguzi Zanzibar, kwa lengo la
kuyapitia tena kwa kina na kushirikisha zaidi wadau ili hatimaye kuweka
msimamo stahiki kabla mapendekezo hayo hayajawasilishwa tena Baraza la
Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa hatua za mwisho za kupitisha
rasmi taarifa ya nchi katika kukuza na kulinda haki za Binadamu.
Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametumia fursa
hiyo kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kulinda na kukuza haki za
bindamu ikiwa ni pamoja na kupokea hoja na maoni ya wadau ili kuboresha
taarifa ya nchi itakayowasilishwa katika Baraza la Haki za Binadamu la
umoja wa mataifa kabla au ifikapo tarehe 9 Septemba, 2016 na kuwataka
watanzania wote kushiriki ipasavyo katika dhana nzima ya kukuza na
kulinda haki za bindamu nchini.
Utaratibu
wa Mapitio kwa kipindi maalum (The Universal Periodic Review) wa
masuala ya haki za binadamu ulianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka
2006 kwa lengo la kuzifanyia mapitio nchi 192 ambazo ni wanachama wa
Umoja wa Mataifa, Tanzania ikiwa miongoni, kwa lengo la kuangalia
utekelezaji wa masuala ya kulinda na kukuza haki za binadamu nchini
mwao.

0 comments:
Post a Comment