Na Sheila Simba-Dar es salaam.
Wapenda
amani nchini wamelaani kitendo cha Jukwaa la Wahariri (TEF)kutoa tamko
dhidi Serikali kuhusu kufungia vituo viwili vya redio hivi karibuni.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Jijini Dar es Salaam, wameonyesha Dhahiri kuchukizwa na TEF na kusema hawajui wanalolifanya.
Bwana
Juma Ramadhan, Mkazi wa Ilala, amesema kuwa hapendezwi na watu kutetea
chombo kinachohatarisha amani Nchi na mali zao kwa kuandika habari za
uchochezi.
“Mimi
nimekaa nchini kwa kipindi kirefu sijaona machafuko je huyu
anayechochea uvunjifu wa amani ana lengo gani kwa Taifa?” aliuliza
Ramadhani.
Naye Bi
Mercy Mwakitalima Mkazi wa Sinza, amesema kuwa Jukwaa hilo linapaswa
kusimamia na kuongoza vyombo wanavyosimamia kutokutumia maneno na lugha
isiyofaa ili kuepeka kuliingiza taifa katika machafuko.
Ameongeza
kuwa wahariri wanapaswa kusimamia maadili ya uandishi wa habari ili
vyombo vyao viandike habari zinazingatia umoja kitaifa uliojengeka kwa
muda mrefu.
“Taifa
letu ni la amani na inatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote,naviomba
vyombo vya habari nchini kuheshimu sheria za Nchi,ki ukweli siku hizi
baadhi ya vyombo wanaongea sana vitu ambavyo havina faida yoyote kwa
jamii, naipongeza Serikali kwa hatua waliochukua ili iwe fundisho kwa
wengine”alisema Mwakitalima
Ameongeza
kuwa sekta ya habari nchini inatakiwa kuwa mstari wa mbele katika
kuhubiri amani na sio kutumia maneno yanayochochea uvunjifu wa amani
kwani kufanya hivyo kutapelekea Taifa pabaya kwa kuwalisha watanzania
vitu visivyofaa.
Kwa
upande Mwalimu wa shule ya Msingi Kinondoni aliyejitambulisha kwa jina
moja la Mwamvua,ameiomba Serikali kuharakisha Muswada habari ili kuwa na
watu wenye sifa pekee katika sekta ya habari kwani kwasasa sekta ya
habari imepoteza umaarufu wake.
“sekta
ya habari nchini kwa sasa haina mwelekeo kila mtu ni mwandishi wa
habari bila hata kuwa na taaluma ya habari hili ni tatizo lazima
Serikali ilifanyie kazi mapema ili kuepeuka kuwa na watu wasiojua
maadili ya kazi hiyo,”alisema Mwamvua.
Naye
Joseph Jeremia ameomba Serikali kuendelea kuvichukulia hatua vyombo vya
habari ambavyo vinamwelekeo wa kuhatarisha amani ya Tanzania kwa
kuvifuta kabisa.
Amesema amani ni rahisi kuipoteza lakini ni kazi ngumu kuijenga kama ilivyo hapa nchini.
Jukwaa
la wahariri walitoa tamko hilo, kufutia Serikali kupitia kwa Waziri wa
Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Nape Nnauye, kutangaza kufungia vituo
viwili vya radio kwa kutangaza habari za uchochezi,ambazo ni Radio five
ya Arusha na Radio Magic fm ya jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment