Mwenyekiti wa Mkutano
wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli (wa tano kutoka kushoto) akiimba wimbo wa Afrika Mashari na
viongozi wenzake wa jumuiya hiyo kutoka Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini, Kenya, Burundi na Rwanda.
Wakuu wa nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiimba wimbo wa Jumuiya hiyo wakiongozwa na
Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati)
wakati wa kikao cha Dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo leo Ikulu jijini Dar es
salaam. Kutoka kulia ni Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Yoweri Museveni wa
Uganda (wa pili kutoka kushoto) na Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto.
Mwenyekiti wa Mkutano
wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
akitoa taarifa fupi ya mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa sasa wa
Jumuiya ya Afrika Masharika (EAC) ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli (kulia) akiongoza kikao cha dharula cha 17 cha nchi za Jumuiya hiyo leo
Ikulu jijini Dar es salaam.Kikao hicho pamoja na mambo mengine kimejadili kuhusu
hali ya amani nchini Burundi na Sudani ya Kusini, ulindaji wa viwanda vya EAC,
Makusanyo ya kodi ya bidhaa toka nje kupitia Mkataba wa EPA na suala la ushuru
na forodha, Kushoto ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Mwenyekiti Jumuiya ya Afrika Masharika (EAC) ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli (kulia) akiteta jambo na Rais wa Mhe. Uganda Yoweri Museveni wakati wa
kikao cha Dharula cha 17 cha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Ikulu jijini
Dar es salaam.
Rais wa Uganda Mhe.
Yoweri Museveni akitoa hotuba fupi kwa wajumbe na wageni mbalimbali waliohudhuria
kikao cha dharula cha 17 cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo Ikulu
jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa
Kenya Mhe. William Ruto akitoa hotuba fupi kwa niaba ya Rais wa Kenya akizitaka
nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kuongeza ushirikiano wakati wa kikao cha dharula
cha 17 cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo Ikulu jijini Dar
es salaam.
Mjumbe maalum wa Rais
wa Sudani ya Kusini Mhe. Aggrey Tisa Sabuni akizungumza kwa niaba ya Rais wa
Sudani ya Kusini Jenerali Salva Kiir Mayardit wakati wa kikao cha dharula cha
17 cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo Ikulu jijini Dar es
salaam. Mjumbe huyo amewashukuru viongozi wa nchi za Afrika Mashariki kwa
kuiruhusu Sudani ya Kusini kujiunga na Jumuiya hiyo.
Rais wa Rwanda Paul
Kagame akitoa salamu zake kwenye mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika
jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu
Mteule wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Christopher Bizivamwo akiapishwa mbele ya
Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki tayari kwa kuanza kutekeleza majukumu ya
Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka 3 wakati wa kikao cha dharula cha 17 cha EAC
kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Balozi Augustino Mahiga
(kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi na Mwakilishi wa Rais wa Burundi
Mhe. Balozi Alain Aime Nyamitwe wakifuatilia kikao cha dharula cha 17 cha
Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Mambo ya
Nje wa Burundi na Mwakilishi wa Rais wa Burundi katika kikao cha dharula cha 17
cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo
Mhe. Balozi Alain Aime Nyamitwe akiwasilisha salam za Rais wa nchi hiyo Pierre
Nkurunzinza.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa salamu zake
kwenye mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Dkt Libérat Mfumukeko akifungua Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi
Wanachama wa Jumuiya hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na baadhi ya wabunge wa Jumuiya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao cha dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Kikao cha dharula cha
17 cha Jumuiya hiyo kikiendelea chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki akiongoza kikao hicho Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Wakuu wa nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wastaafu wa Tanzania na wale wa Jumuiya hiyo mara baada ya kumalizika kwa kikao
cha dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam
leo.
Mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakijadiliana masuala mbalimbali mara
baada ya kumalizika kwa Kikao cha dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo kilichokuwa
kikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt.John
Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya Mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakifuatilia Kikao cha dharula cha 17
cha Jumuiya hiyo kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye
ni Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo. Picha/Aron
Msigwa na Hussein Makame.
0 comments:
Post a Comment