Home » » Zaidi ya Shilingi Milioni thelathini za kusanywa katika kuwasaidia wa athirika wa Tetemeko la Ardhi Kagera

Zaidi ya Shilingi Milioni thelathini za kusanywa katika kuwasaidia wa athirika wa Tetemeko la Ardhi Kagera

 
Na Anitha Jonas – whusm

Dar es Salaam.
 
Zaidi ya Shilingi Milioni thelathini za kusanywa katika kuwasaidia wa athirika wa Tetemeko la Ardhi Kagera.
Kiasi hicho cha Pesa kilikusanywa jana jijini Dar es Salaam katika Harambee iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa ajili ya  ilikuwasaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.
Akizungumza katika ufunguzi wa Harambee hiyo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye aliwataka watanzania kulichukulia suala  Maafa ya Tetemeko la Ardhi Mkoani  Kagera kuwa nila kila mtanzania na kutoa wito wakujitoa kuchangia chochote kunusuru hali ya watu waliyoathirika pamoja na miundombinu.
“Ninawaomba  watanzania wote na wasio watanzania kujitokeza kutoa misaada kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko hili,pia ombi langu kwa wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia kuboresha miundombinu iliyoharibika ikiwemo,Shule,Barabara na Makazi ya wananchi wa Kagera kwa kufanya hivyo kutasaidia kurudisha furaha kwa wakazi hao,”alisema Mhe.Nnauye.
Akiendelea kuzungumza katika Harambee hiyo Mhe.Nnauye alipongeza  uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa kuandaa Harambee hiyo  kwani kwa kufanya hivyo wameonyesha kuguswa na maafa hayo ya Tetemeko.
Kwa upande wa mmoja wa wadau waliyohudhuria harambee hiyo kutoka Kampuni ya Startimes  Bw.Juma Sharobaro alitoa wito kwa watanzania kuungana kwa umoja na kuwasaidia waathirika hao wa tetemeko kwa kutoa mfano wanchi yao ya China kuwa ilishawahi kupatwa na maafa ya tetemeko kama hilo na liliuwa watu wengi lakini walijiunga kwa umoja kutoa msaada kwa waathirika.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa  (TBC) Dkt.Ayoub Rioba alisema kuwa Harambee hiyo ni endelevu na aliwasihii watanzania kujitokeza na kuchangia kwa kiasi chochote kulingana na uwezo wako kwani haba na haba  hujaza kibaba na uhitaji wa msaada mkoani Kagera ni mkubwa.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa Shirika la Utangazaji la Taifa alizitaja namba ambazo mtu yeyeto anaweza kutuma mchango wake kuanzia jana kuwa kwa upande wa benki ni kupitia Akaunti ya namba ya CRDB Benki ambayo ni 15222561730,Tigopesa 0718 069616,Mpesa 0768 196 669 na Airtel Money 0682 950009 na kusema kwa kuchangia kiasi chochote kupitia namba hizo kutawasaidia sana wakazi wa Kagera.
Hata hivyo ilielezwa kuwa msaada wowote unapokelewa na shirika hilo ukiwemo wa vyakula na mahitaji mengine ambayo mtu yoyote atakuswa kuchangia kwa wakazi hao.
                     
                           *******************MWISHO******************


0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa