Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » TPDC yakabidhi msaada wa Viti 142 kwa Shule ya Sekondari Kisungu.

TPDC yakabidhi msaada wa Viti 142 kwa Shule ya Sekondari Kisungu.


Na Daudi Manongi,MAELEZO.
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) limekabidhi msaada wa Viti 142 kwa shule ya Sekondari Kisungu iliyopo Tabata Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi msaada huo leo Jijini Dar es Salaam Meneja Mawasiliano wa TPDC alisema taasisi hiyo imeamua kuunga mkono  jitihada za Rais  wa Jamhuri wa Muungano  wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli  za kupunguza  uhaba wa  madawati katika shule za Msingi na Sekondari nchini.
“TPDC inaunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli katika kumaliza tatizo la wanafunzi kukaa chini, tumeamua kutekeleza kwa vitendo jitihada hizo” alieleza Msellemu.
Aidha Msellemu alisema kwa kipindi kirefu TPDC imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia huduma za kijamii nchini ikiwemo elimu na afya, ambapo hivi karibuni taasisi hiyo ilijenga zahanati pamoja na kukabidhi Madawati 500 katika kata ya Madimba iliyopo Mkoani Mtwara.
Akipokea msaada wa viti hivyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisungu, Mkamo Mgeta aliishukuru TPDC kwa msaada ambao umelenga kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli na kuwataka wadau zaidi kujitokeza kusaidia uhaba huo.
MWISHO.0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa