Na Ally Daud
MAELEZO
Dar es Salaam
11.12.2016
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (2017-22) wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto (Maendeleo ya Jamii) Bi. Siaba Nkinga katika mkutano na
waandishi wa habari, ambapo alisema uzinduzi huo unatarajia kufanyika
Desemba 13 mwaka huu Jijini Dar es Salaam
“Mpango
huu jumuishi wa miaka mitano utakaouzinduliwa umezingatia nguzo kuu
mbili, ambazo ni kuzuia na utoaji wa huduma kwa wahanga wa vitendo vya
ukatili wa kijinsia” alisema Bi. Nkinga
Alisema kuwa mpango kazi huo unatarajiwa kutoa msukumo mpya katika kuwezesha utekelezaji majukumu ikiwemo kutetea, kushauri na kutoa elimu kwa umma ili kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu athari za ukatili kwa wanawake.
Kwa mujibu wa Nkinga alisema kuwa utafiti
uliofanywa na Shirika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni (UNICEF) wa mwaka
2015, unaonyesha kuwa Tanzania ina asilimia 3.5 ya watoto wa umri wa
miaka 7 – 17 walio nje ya shule kutokana na sababu mbalimbali za ukatili.
Alibainisha Vitendo
vya ukatili wa kijinsia vilivyoshamiri zaidi ni pamoja na vipigo,
ubakaji, ulawiti, mauaji ya vikongwe, na watu wenye ualibino,
usafirishaji haramu wa binadamu, kutelekeza familia, udhalilishaji,
ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment