Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameitaka jamii kuwasaidia watu
wenye ulemavu ili waweze kujiajiri na kukabiliana na hali ngumu ya
maisha.
Dkt.
Mpango ametoa rai hiyo wakati alipotembelea banda la mlemavu asiyeona,
Bw. Abdalah Nyangalilo, ambaye amewakusanya watu kadhaa wenye ulemavu na
kuwapatia mafunzo ya ushonaji nguo katika maonesho ya kwanza ya viwanda
vya ndani, yanayofanyika katika Uwanja wa maonesho ya biashara wa
Mwalimu J. K. Nyerere, barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.
Waziri
huyo wa Fedha na Mipango, ambaye ametoa msaada wa vyerehani viwili ili
kuwaongezea nguvu, amesema kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kufanya
mambo makubwa ya kijasiliamali yatakayo wasaidia kujikimu kimaisha,
endapo jamii itajitolea kuwasaidia kwa hali na mali
0 comments:
Post a Comment