Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa Serikali imeanza
kuyafanyia kazi maoni na malalamiko ya wafanyabiashara na wawekezaji kwa
ujumla kuhusu kodi zinazolalamikwa kwa lengo la kuhuisha ama kubadili
kodi zinazoonekana kuwa ni kero
Dkt
Mpango amesema hayo mara baada ya kutembelea na kukagua maonesho ya
kwanza ya viwanda vya ndani, yanayofanyika katika Uwanja wa maonesho ya
biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, barabara ya Kilwa, Jijini Dar es
salaam.
Amewataka
wafanyabiashara na wawekezaji kuwasilisha maoni yao kuanzia mwezi huu
wa Desemba wakati ambapo Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango,
iko katika mchakato wa kuandaa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018.
0 comments:
Post a Comment