Wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mpigapicha
Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku baada ya kutolewa
heshima za mwisho katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es
Salaam, tayari kulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi.
(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwaongoza
waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mpigapicha
Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku katika Uwanja wa Shule
ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam. Mwili wa Mpoki ulisafirishwa kwenda
kwao Msalato Dodoma kwa mazishi.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa akiwa
ameshika shada la maua alipokuwa akiingiza kwenye gari lenye jeneza la
mwili wa marehemu Mpoki Bukuku
Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo ambaye pia ni Mmiliki wa Blog
hii, Richard Mwaikenda akitoa salamu za rambirambi za Chama cha Mabloga
Tanzania (TBN) wakati wa kuaga mwili wa mpendwa Mpoki Bukuku.
Mwakilishi wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Habari Tanzania (MOAT), Saed Kubenea akitoa salamu za rambirambi
Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akitoa salamu za rambirambi
Mwakilishi wa Chama cha Wapigapicha za Habar Tanzania (PPAT), Selemani
Mpochi akitoa salamu za rambirambi. Mpoki alikuwa mwanachama wa chama
hicho.
ADMIN wa Group la WhatsApp la Tasnia, Thomson Kasenyenda akita salamu
za rambirambi na kuahidi group hilo kuwasilisha mchango wao kwa kulipia
ada za shule za watoto wa marehemu
Mwenyekiti wa Chama cha Bongo Movie, Steven Nyerere akitoa salamu
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo na Burudani
Tanzania (TASWA), Juma Pinto akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mpoki
Bukuku.
Benny Kisaka akitoa heshima za mwisho
Mhariri Mtendaji wa The Guardian, Mgamba akitoa heshima za mwisho
Mmiliki wa Blog ya Michuzi, Muhidini Issa Michuzi akitoa heshima za mwisho
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mpoki Bukuku
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete akitoka kutoa heshima za mwisho
Mpigapicha wa The Guardian na Nipashe akisaidiwa baada ya kutoa heshima za mwisho
Mpigapicha wa zamani wa Daily News, Athuman Khamisi akitoa heshima za mwisho
Mtoto wa kike wa maraehemu Mpoki Bukuku akimvalisha Rozali wakati wa kuaga mwili wa babake
Mjane wa marehemu Lillian akiubusu mwili wa mumewe
Mtoto wa kiume wa marehemu Mpoki Bukuku, Junior akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa babake
Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Msalato Dodoma kwa mazishi.
0 comments:
Post a Comment