Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda akimfariji
mjane wa marehemu Mpoki Bukuku, Lilian nyumbani kwa marehemu, Tabata
Bwawani, Dar es Salaam. Bukuku alifariki juzi baada ya kugongwa na gari
Barabara ya Bagamoyo karibu na Kituo cha ITV, Mwenge. PICHA NA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kibanda akimfariji mama mzazi wa marehemu Mpoki Bukuku
Kiongozi wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe (kulia) akizungumza jambo na
Shemeji wa marehemu Mpoki Bukuku, Edwin Mjwahuzi alipokwenda kuwafariji
wafiwa nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani.
Zitto Kabwe (kulia) akizungumza na kaka wa Marehemu Mpoki, Gwamaka Bukuku wakati wa msiba huo
Waandishi wa habari wakiwa kwenye msiba wa marehemu Mpoki Bukuku ambaye
alikuwa Mpigapicha mwandamizi wa magazeti ya Kampuni ya The Guardian
Wanahabari wakijadiliana mambo wakati wa msiba huo
Mmmiliki wa Blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda, ambaye pia ni
Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Lelo, Kamanda Richard Mwaikenda
(kulia) akiwa na wanahabari wenzie kwenye msiba huo.Kutoka kushoto ni
Mpigapicha wa Waziri Mkuu, Hilary Bujiku, Mmiliki wa Blog ya K-VIS,
Khalfan Said, Mmiliki wa Blog ya Michuzi, ambaye pia ni Mpiga Piacha na
Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Muhidini Issa Michuzi, Mpigapicha
Mkuu wa Gazeti la Mwananchi, ambaye ni shemeji wa marehemu Mpoki, Edwin
Mjwahuzi na Francis Chirwa ambaye ni mmoja wa viongozi wa Bodi ya
Wahariri wa Gazeti la Raia Mwema. ,
Waombolezaji wakiwa kwenye msiba
Jirani rafiki wa karibu wa marehemu, Mpoki, maarufu kwa jina la Mijisu akilia wakati wa msiba
0 comments:
Post a Comment