Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » NEC yakutana na ugeni kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani

NEC yakutana na ugeni kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Christina Njovu, NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imepokea ujumbe Taasisi ya  Tume za Uchaguzi Duniani (AWEB) uliokuja kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya uendeshaji Uchaguzi.
Ujumbe huo umekuja  kujifunza kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) juu ya masuala mbalimbali ya uendeshaji Uchaguzi nchini ikiwemo matumizi ya vifaa vya kuandikishia wapiga kura.
Mkurugenzi wa Mipango na Oparesheni  Bw. Lee Ju-Hwan  alisema  kuwa yeye na ujumbe wake wamekuja kubadilishana uzoefu katika technolojia ya Kuandikisha Wapiga Kura.
Ujumbe huo umekutana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani na kufanya mazungumzo naye ofisini kwake baada ya kukutana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya tume hiyo kutembelea ofisi mbalimbali za Tume hiyo na kujifunza.
Wakiwa katika kikao na baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ujumbe huo wa watu watatu ulijifunza namna mashine ya Biometric Voter Registration (BVR) inavyofanya kazi na jinsi NEC ilivyoweza kuandikisha Wapiga Kura wengi kwa kutumia mashine technolojia hiyo  na changamoto zake.
Aidha ujumbe huo  umekuja na aina mpya  ya technologia ambayo inauwezo wa kuandikisha Wapiga Kura, kutuma taarifa za Wapiga katika kanzidata kutoka katika kituo cha kujiandikishia na  kuhakiki Wapiga Kura siku ya Uchaguzi .
Mashine hiyo ambayo ni ndogo ukilinganisha na ile BVR ina uwezo wa kutumiwa na mtu mmoja ambaye ataweza kumuandikisha Mpiga Kura katika hatua zote hadi kupata kitambulisho cha mpiga Kura na inabebeka kirahisi.
Ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Mipango na Operesheni Lee Ju-Hwan, Mtafiti Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi Park Jae Sumg.
Technologia hiyo mpya inaweza kurahisisha utendaji kazi katika masuala ya uandikishaji wapiga Kura, kuhakiki wapiga kura na kutuma taarifa katika kanzi dara.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa