Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia
salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg. Mwishehe
Shaban Mlao kufuatia
kifo cha Profesa Idrissa Ali Mtulia, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Rufiji
kilichotokea jana tarehe 05 Desemba, 2016 jijini Dar es salaam.
Prof
Mtulia ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama
na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mbunge wa
Jimbo la Rufiji, Katibu Mkuu wizara mbalimbali, Daktari wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili na Mwenyekiti wa Bodi ya
Madawa (MSD)
Prof
Mtulia, atakumbukwa na wanachama wa CCM na Wananchi wa Mkoa wa Pwani
kwa jitihada zake za ujenzi na uimarishaji wa Chama na mchango wake
mkubwa katika maendeleo ya Wananchi wa Rufiji.
Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu.
Imetolewa na:-
Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
06.12.2016
0 comments:
Post a Comment