NA BEATRICE LYIMO NA GEORGINA MISSAMA- MAELEZO-DAR ES SALAAM.
Serikali
imetoa wito kwa wasanii nchini kurasimisha kazi zao ili kuweza
kutambulika, kupata haki zao na kuongezea pato lao na la taifa.
Wito
umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura wakati wa Mkutano na
waandishi wa habari ulikuwa unahusu ubunifu wa vipaji na jinsi ya
kuviendeleza.
“Sanaa
inaongeza uelewa, sanaa ni chanzo kikubwa cha ajira hasa kwa vijana
inayopelekea kukua kwa pato la taifa ingawa kuna changamoto kwa wasanii
kutojitokeza au kujisajili ili kuweza kutambulika katika jamii”,
alifafanua Naibu Waziri Wambura.
Alisema
kuwa ili kutekeleza agizo la Rais wakati wa hotuba ya uzinduzi wa Bunge
kuhusu haki za wasanii nchini, Wambura aliwataka wadau mbalimbali wa
sanaa na sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha
maslahi ya wasanii yanaboreshwa na kupinga uharamia wa kazi za wasanii.
Aidha,
Wambura aliwataka wasanii kufuata Sheria, Kanuni na taratibu kwa
kushirikiana na taasisi zinazohusika na masuala ya sanaa ikiwemo Tasuba,
Basata, Cosota, Bodi ya Filamu ili kuwawezesha kufanya kazi kwa unafuu.
“Kama
tunataka maendeleo ya kweli ni lazima kuthubutu, unapokuwa huna lengo
au ndoto ni mkasa mkubwa katika jamii hivyo tunapaswa kuwa na ndoto
zinazopelekea maendeleo yetu” alifafanua Wambura.
Kwa
upande wake Rais wa Taasisi ya TCDB Mwalimu Calorus Bujimu, alisema
kuwa taasisi imeandaa programu ya kukuza kazi za wasanii nchini kwa
lengo la kuibua vipaji vya wasanii na kuvikuza.
Alisema
kuwa uanzishwaji wa programu hiyo ni matokeo ya utafiti yaliyobaini
kuwa uwepo wa wasanii wengi wenye vipaji katika Nyanja mbalimbali za
sanaa, lakini wanakabiliwa na changamoto za kiuchumi na kukosa ubunifu.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment