Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 |
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga (katikati) akizungumza na watumishi wa Wizara hawapo
pichani, kwenye kikao cha pamoja kilichofanyika leo katika ukumbi wa
kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Dkt. Aziz P. Mlima na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na
Rasilimali watu, Bw. Hamid Mbegu. |
 |
Sehemu
ya Wakurugenzi wakifuatilia kikao, kutoka kushoto Mkurugenzi wa Idara
ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya
Afrika, Balozi Samuel Shelukindo, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya
Kati, Balozi Abdallah Kilima na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi
Baraka Luvanda. |
 |
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi, katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Stephen
Mbundi, Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji
wa Wizara, Bi. Mindi Kasiga na koshoto ni Mratibu wa dawati la mafunzo,
Bi. Tagie Mwakawago. |
 |
Watumishi wakifuatilia kikao. |
 |
Sehemu ya watumishi wakifuatilia kikao. |
Sehemu nyingine ya watumishi wakifuatilia kikao.
===============================================
Wakati
huo huo uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki umetumia fursa hiyo kutoa zawadi kwa Idara na vitengo
vilivyofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka 2016.
 |
Balozi Mbelwa Kairuki akionyesha zawadi mara baada ya kukabidhiwa na Waziri Mahiga. |
 |
Mkurugenzi
wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Mbundi akipokea zawadi ya
Idara ya zilizofanya vizuri. Pamoja na Idara hizo Idara nyingine
zilizoingia tano bora ni pamoja na Idara ya Amerika na Ulaya, Idara ya
Afrika na Kitengo cha Fedha na Uhasibu. |
 |
Mfano wa Zawadi iliyokabidhiwa kwa Idara na vitengo vilivyoshinda na kuingia katika tano bora. |
 |
Kikao kikiendelea. |
0 comments:
Post a Comment