Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
MOJA
ya malengo makuu ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuongeza nguvu katika
ukusanyaji wa mapato nchini kwa lengo la kupanua wigo katika ukusanyanyi
wa kodi ili kuimarisha mfumo wa utoaji huduma kwa wananchi.
Akifungua
mkutano wa Bunge la 11 la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mwaka jana
mjini Dodoma, Rais Dkt. John Pombe Magufuli alisema Serikali yake
itaongeza nguvu katika upanuzi wa wigo wa kodi na kuongeza ufanisi
katika ukusanyaji wa mapato.
Rais
Magufuli alisema, Serikali yake itahakikisha kila mtu anayestahili
kulipa kodi analipa kodi stahiki kwa maendeleo ya nchi.
“Hatutasita
kumchukulia hatua mtu yoyote atakayekwepa kulipa kodi, tunawaomba
wananchi mhakikishe mnapewa risiti kila mnaponunua bidhaa au huduma.
Kodi ni kitu muhimu kila mtu anayestahili kulipa kodi alipe” alifafanua
Rais Magufuli.
Aidha,
alisema kuwa Serikali yake itahakikisha kila senti inayoongezeka katika
mapato ya Serikali inaelekezwa katika kutoa huduma bora zaidi kwa
wananchi na kuziba mianya ya upotevu wa fedha za Serikali ambayo
inapunguzia uwezo wa kuhudumia wananchi.
Taarifa
ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inamtaka kila Mfanyabiashara
anayetumia mashine ya EFD anayekwepa kutoa risiti ni kosa la kisheria
ambapo adhabu yake ni kulipa faini isiyopungua sarafu ya pointi 100 hadi
pointi 150 ya thamani halisi ya fedha au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Aidha
kwa mtu yeyote atakayeshindwa kudai au kutoa taarifa ya kukataliwa
kupewa risiti au ankara ya malipo ya bidhaa au huduma atakuwa ametenda
kosa na ikithibitika atatozwa faini isiyopungua sarafu ya pointi 2 na
zisizozidi sarafu ya pointi 100.
Hata
hivyo kila mfanyabiashara aliyesajiliwa na kodi ya Ongezeko la la
Thamani anatakiwa kuzingatia kutumia mashine za kodi za kielektroniki
(EFD).
Hivyo
basi Utii wa Sheria bila shuruti katika masuala ya kutoa na kudai
risiti pindi tununuapo bidhaa ni jukumu letu sote na hivyo kupelekea
ongezeko la mapato kwa maendeleo ya Taifa letu.
Aidha
dira ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni kuongeza mapato ya ndani
kwa kuimarisha ulipaji wa kodi kwa hiari, hivyo watanzania wenzangu
tushirikiane na Mamlaka hiyo katika kuongeza mapato ya ndani kwa
maendeleo ya Taifa.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment