BEN MWAIPAJA -WFM
DAR ES SALAAM, 25 JAN 2017
BENKI
ya Dunia imekubali kuikopesha Tanzania fedha kwaajili ya miradi
mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mkopo wa Dola Milioni 350 kwa ajili ya
Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Dar es salam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango, amewaambia waandishi wa
Habari mara baada ya kumalizika kwa Mazungumzo kati yake na Makamu wa
Rais wa Benki ya Dunia anaye shughulikia Kanda ya Afrika, Mhe. Makhtar
Diop, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Amesema
kuwa kukamilika kwa upanuzi wa Babdari hiyo kutasaidia kuongeza ubora
wa huduma zinazotolewa na Bandari hiyo hatua itakayo chochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
0 comments:
Post a Comment