Na: Frank Shija - MAELEZO
Mwili
wa aliyekuwa Mgombea wa kwanza Mwanamke kuwania kiti cha Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Anna Senkoro unatarajiwa kuzikwa
katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi
tarehe 07/01/2017 kuanzia saa 8:00 mchana.
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Bwana. Fred Sendim ambaye ni Msemaji wa Familia ya marehemu Dkt. Senkoro.
“Mipango
ya mazishi inaendelea vizuri nyumbani kwake Segerea, pia nitumia fursa
hii kutoa shukrani za kipekee kwa wote wanaoendelea kutufariji na
kushirikiana nasi bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.” Alisema
Sendim.
Msemaji
huyo wa familia amesema kuwa taratibu za mazishi zitataunguliwa na
Ibada maalum itakayoambatana na utoaji wa heshima za mwisho kuanzia saa Saba mchana katika Kanisa la Winners lililopo Banana, Ukonga jirani na Kituo cha Mafuta cha Oil Com.
Awali
akielezea kifo chake msemaji wa familia hiyo amesema kuwa marehemu
alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo ambapo juzi tarehe 04 majira
ya saa 11 alfajiri alizidiwa na kupelekwa Hospitali kwa ajili ya
matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na baadaye
alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alifikwa na mauti mnamo
saa 3:30 asubuhi.
Dr.Anna
Senkoro alikuwa mgombea wa kwanza mwanamke kuwania kiti cha Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kupitia Chama cha APPT
Maendeleo, Marehemu ameacha watoto wa tatu na wajukuu wa wiwili.
Mungu hailaze roho ya Maerehemu mahali pema peponi amina.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment