Na Adili Mhina, Dar.
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango imefanya ziara
katika Mradi wa ujenzi wa Barabara za juu (Flyovers) unaoendelea katika
makutano ya barabara za Nyerere/Mandela Jijini Dar es salaam na
kuelezwa kuwa utekelezaji wake umefikia asilimia 19.2.
Ziara
hiyo iliyofanyika hivi karibuni kwa lengo la kuangalia maendeleo ya
mradi huo ilitoa fursa kwa Bw. Kiyokazu Tsuji, Mhandisi Mkazi kutoka
Kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui ambayo ndiyo inayotekeleza ujenzi
huo kueleza maendeleo ya ujenzi kwa wataalam kutoka Tume ya Mipango.
Mhandisi
huyo alieleza kuwa malengo ya awali yalielekeza kuwa hadi kufikia
mwishoni mwa mwezi Novemba 2016, utekelezaji uwe umefikia asilimia 21.2
lakini lengo hilo halikufikiwa kutokana na moja ya mashine kupata
hitilafu na kulazimika kuagiza wataalam kutoka nje ya nchi kuja
kuifanyia matengenezo.
Hata
hivyo Mkandarasi huyo alieleza kuwa tayari wamejipanga vizuri katika
kuhakikisha wanafidia muda uliopotea wakati mashine hiyo ilipokuwa
haifanyi kazi ili ujenzi wa barabara hizo ukamilike ndani ya muda
uliopangwa.
Nao
walaalam kutoka Tume ya Mipango walieleza kuwa Serikali na Wananchi kwa
ujumla wanatarajia kuwa ujenzi huo utakamilika kwa muda uliopangwa
hivyo Mkandarasi huyo ana wajibu wa kufanya kila linalowezekana ili
mradi huo ukamilike kwa wakati.
Wataalamu
hao pia walimshauri Mkandarasi huyo kuwa ni vyema akawapeleka nje
wataalam wanaoziendesha mashine hizo ili waweze kupata ujuzi na uwezo wa
kutengeneza mitambo pale inapohitajika badala ya kusubiri watu kutoka
nje kuja kufanya kazi hiyo.
Walieleza
kuwa kuwepo kwa wataalam wa ndani wenye uwezo wa kutatua hitilafu
zinazojitokeza katika mitambo itasaidia kupunguza gharama na kuokoa muda
ili kufanya mradi uende bila kusimama.
Ujenzi huo unaotekelezwa kwa miezi 35 kauanzia Disemba 1, 2015 hadi Oktoba 31, 2018 unalenga kupunguza tatizo la msongamano wa magari na kuboresha huduma za usafiri katika Jiji la Dar es Salaam.
MWISHO
Captions
1. Mhandisi
Mkazi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui, Bw.Kiyokazu Tsuji
(wa kwanza kulia) akionesha hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa
Barabara za juu (Flyovers) eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam. Pembeni
yake ni kiongozi wa timu ya ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango,
Mhandisi Omari Athuman.
2. Kiongozi
wa timu ya ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Omari
Athuman (mwenye shati ya mikono mifupi) akitoa ushauri kwa wahandari
wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa bararabara za juu jijini Dar es Salaam.
3. Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
4. Mhandisi Omari Athuman (kulia) akiongea na Ofisa Mshauri wa masuala ya usalama kazini, Bw.
Richard Barwan wakati wa ziara ya Timu ya Mipango katika mradi wa
ujenzi wa Barabara za juu eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
5. Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
6. Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
________________
Adili Justine Mhina,
Information Officer,
Information Officer,
Ministry of Finance and Planning,
Planning Commission,
Box 9242,
Dar es Salaam.
Tel 2112681-4/2127122
Fax 2115519/2117103
Mob 255-787 677 881
Box 9242,
Dar es Salaam.
Tel 2112681-4/2127122
Fax 2115519/2117103
Mob 255-787 677 881
0 comments:
Post a Comment