NA MAGRETH KINABO - MAHAKAMA YA TANZANIA
07/01/217
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza Majaji wanawake na Mahakimu wa Wanawake nchini kuendelea kutoa elimu na ujuzi juu ya haki za binadamu ili kuwezesha jamii kuepukana na vitendo rushwa,ikiwemo rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu huyo wa Rais aliyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane Mkutano wa Nane wa Mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) uliofanyika jijini Dar es salaam, ambao umehusisha Majaji Wanawake, Mahakimu Wanawake, wakiwemo baadhi Wanaume.
Mkutano huo wenye lengo la kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya utoaji haki na hukumu bila ubaguzi. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Kuongoza njia kufikia
hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati”
hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati”
Aliongeza kwamba chama hicho kina wajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa haki bila ubaguzi , hususan kwa masuala yanayohusu wanawake na watoto ili kuwezesha ustawi wao kwa ujumla na maendeleo ya nchi.
“ Ninakiaagiza Chama hiki kuendelea kutoa elimu juu ya haki za binadamu katika jamii kwa maafisa wa Mahakama, watunga sheria na kwa watu waliathirika na vitendo vya rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia kwa kuwa utoaji wa elimu ndio , utawezesha upatikanaji wa haki kwa wakati kwa jamii inayohitaji ,” alisema Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aliongeza kwamba chama hicho kina wajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa haki bila ubaguzi , hususan kwa masuala yanayohusu wanawake na watoto ili kuwezesha ustawi wao kwa ujumla na maendeleo ya nchi.
Aidha Makamu huyo wa Rais amekishukuru Chama cha Majaji Wanawake cha Dunia(IAWJ) kwa michango na msaada wake kwa TAWJA kwa program ya miaka mitatu ya ya kupambana na vitendo vya rushwa ya ngono vinadaiwa kufanywa na baadhi ya watu wenye madaraka.
Alisema vitendo hivyo vinasababisha baadhi ya wanawake kutopata huduma mbalimbali zikiwemo za elimu, ajira, haki na huduma nyinginezo.
Makamu
wa Rais pia ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria, Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (UN Women) na wadau
wengine wa TAWJA kwa kuunga mkono mapambano ya aina zote za ubaguzi na
ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.
0 comments:
Post a Comment