Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KICHINA.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KICHINA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



NA Daudi Manongi -  MAELEZO.
17/01/2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 21 na 22 January 2017 kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 11 Jioni.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa China nchini Bw.Gao Wei alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari.

Amesema mwaka huu utafahamika kama mwaka wa Jogoo wenye kuweka mtazamo mkubwa Afrika huku yakiambatana na burudani nyingi kutoka kwa vikundi mbalimbali vya sanaa kutoka China na nchini,maonyesho ya picha,vyakula vya kichina na maonyesho mbalimbali ya kibiashara.

Katika maadhimisho hayo makampuni 60 yatashiriki katika kuonyesha bidhaa mbalimbali,pia nchi 150 na majiji 400 yatasherehekea maadhimisho haya ya mwaka mpya.

Akizungumzia mahudhurio ya siku hiyo Bw.Wei amesema kuwa wanategemea ushiriki wa watu zaidi ya 6000 katika maadhimisho hayo ya siku mbili ambayo yanasisitiza zaidi urafiki na mshikamano.

Katika kufanikisha maadhimisho hayo Kampuni za HUAWEI na CRDB Benki zimejitokeza kudhamini maadhimisho ya mwaka huu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa