Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Jeshi
la Polisi Tanzania limeondoa taa za ziada (spot light) 665 zilizokuwa
zimewekwa kwenye baadhi ya magari bila kupata kibali na utaratibu wa
mtengenezaji wa chombo husika.
Hatua hiyo inalenga kupunguza ajali za barabarani zinazosababishwa na matumizi ya taa hizo zisizo sahihi.
Takwimu
hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kikosi
cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu matumizi ya taa za gari.
DCP
Mpinga alisema kuwa marekebisho yoyote katika gari yanahitaji kibali
cha mtengenezaji , kinyume cha hapo ni uvunjaji wa sheria.
Aliongeza
kuwa taa hizo hutumika vibaya hasa nyakati za usiku na kuwa chanzo cha
ajali kwa sababu zinapotumika hupoteza uwezo wa mtumiaji kuzitawala kwa maana ya kubadilisha uwakaji wake.
Kamanda
Mpinga aliwashukuru baadhi ya watumiaji wa barabara kwa kuunga mkono
usimamizi wa sheria kwa kuziondoa taa hizo kwa hiari na kuwasisitiza
kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo waendelee kuzitoa taa hizo wenyewe.
Aidha,
Kamanda huyo alitaja ajali za barabarani zilizotokana na matumizi
mabaya ya taa kwa mwaka 2015 zilikuwa 104 na mwaka 2016 zilikuwa 123.
mwisho
0 comments:
Post a Comment