Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja ambapo anatarajia kufanya shughuli mbali mbali na kuwatubia wananchi katika mkutano wa hadhara .
Kwa mujibu wa wa taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja generali mstaafu Raphael Muhuga Waziri Mkuu atawasili leo majira ya saa tatu na nusu katika uwanja wa ndege wa Mpanda .
Mara baada ya kuwasiri katika uwanja wa ndege wa Mpanda ataelekea Ikulu ndogo ya Mpanda ambako atasomewa taarifa ya Mkoa katika Ikulu ndogo .
Muhuga alisema kisha Waziri Mkuu ataelekea katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambako atafungua rasmi duka la kuuza dawa la MSD ambalo aliagizo mwaka jana lifunguliwe kwenye hospitali hiyo .
Baada ya kufungua duka la dawa ataelekea uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili ambako atakabidhi hundi ya ruzuku kwa wachimbaji wa dogo wa madini 59 wanatoka Mikoa yote ya hapa nchini .
Alisema mara baada ya kukabidhi hundi hizo wachimbaji wadogo zilizotolewa na Serikali kwa ajiri ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kununulia vifaa atawahutubia Wananchi wa Mkoa wa Katavi kwenye uwanja huo wa Kashaulili .
Meja Generali Mhuga alieleza baada ya kuwahudia wakazi ataondoka Mkoani Katavi siku hiyo hiyo ya kesho na kuelekea Mkoani Dodoma majira ya saa tisa alasiri.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment