Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi amewaasa
wafugaji kuacha kuingiza mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza
hifadhi hizo.
Katibu Mkuu uyo aitoa wito huo wakati akizungumza baada ya kufanya matembezi ya kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff ambapo wageni mashughuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa alishiriki.
“Hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya wanyama pori pekee na siyo kwa mifugo na hivyo kila mwananchi analo jukumu la kuyalinda mazingira haya,”Aliongeza Mej.Gen Milanzi.
Awali
akizungumza katibu mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina mkakati mkubwa
wa kuhakikisha inashirikiana na nchi zingine katika kutokomeza kabisa
Ujangili wa pembe za ndovu nchini.
Aidha
aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuwa mstari wa
mbele katika kupambana na ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo upigaji marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizo ifikapo mwezi machi Mwaka huu.
Mbali
na hayo katibu Mkuu uyo amewaasa watanzania kuwafichua wale wote
wanaojihusisha na biashara hiyo na kuonya kuwa kwa kushiriki katika
biashara hii tutawafanya tembo wetu kuwa historia kwani hawatakuwepo
tena.
Naye Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa amewataka
watanzania kulinda na kutunza mbuga zetu kwani ni urithi wa kila
mtanzania na kuzitaka nchi mbalimbali kusaidia katika kulinda urithi huu
wa wanyama na kuvitaka vyombo vya habari kushiriki vyema katika
kutangaza mbuga zetu na pia kutangaza jitihada zinazofanywa na serikali
katika kutokomeza ujangili wa pembe za ndovu.
0 comments:
Post a Comment