Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SERIKALI KUANDAA SERA YA LUGHA.

SERIKALI KUANDAA SERA YA LUGHA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akisalimia na Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh alipowasilia katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere katika kongamano la Lugha ya Kiswahili.


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akisalimia na Waziri zamani wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Mohamed Seif Khatib wakati alipowasili katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere kufungua kongamano la Lugha ya Kiswahili.


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akiweka saini katika kitabu cha wageni mara alipowasilia katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere katika kongamano la la Lugha ya Kiswahili.


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati) akielekea katika Ukumbi wa Utamaduni katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere kufungua kongamano la Lugha ya Kiswahili. kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere( Mipango Fedha na Utawala) Dkt. Magreth Shawa na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh


Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Shani Kitogo akiimba ushairi katika ufunguzi wa kongamano la la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.  


Bw. Sarungi Innocent akisoma risala kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura(hayupo Pichani) kwa niaba ya Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) wakati wa ufunguzi wa kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.  


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akipokea Risala kutoka kwa Bw. Sarungi Innocent aliyesoma risala kwa niaba ya Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) wakati wa ufunguzi wa kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.  


Mlezi wa Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) na Waziri zamani wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Mohamed Seif Khatib akitoa mada mbalimbali kuhusu Lugha ya Kiswahili katika kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.   


Mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Riwaya Bw. Shafi Adam Shafi akitoa mada mbalimbali kuhusu Lugha ya Kiswahili katika kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.    


Mwenyekiti wa Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh akitoa maelezo kuhusu Chama chake katika kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.    


Naibu Mkuu wa Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere (Mpango Fedha na Utawala) Dkt. Magreth Shawa akieleza kuhusu Chuo chake katika kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.    


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akizungumza na washiriki wa kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.  

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akipongezwa na Mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Riwaya Bw. Shafi Adam Shafi mara baada ya kumaliza kuzungumza na kufungua rasmi kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.    


 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika katika  kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.  

Baadhi ya washiriki wakiangalia vitabu mbalimbali katika maonesho ya vitabu yaliyofanyika sambamba na kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.          
Picha na habari na Raymond Mushumbusi

Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imeanza rasmi kuandaa Sera ya Lugha ambayo itatoa muongozo kwa taifa kuhusu masuala yote ya maendeleo ya Lugha nchini ikiwemo Lugha ya Taifa ya Kiswahili.
 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura wakati akifungua kongamano la Lugha ya Kiswahili liliofanyika katika Chuo cha KumbuKumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini Dar es Salaam.


Mhe. Anastazia Wambura amesisitiza kuwa kwa kipindi kirefu sana kumekuwa na uhitaji wa Sera ya Lugha ambayo itasaidia katika ukuaji na matumizi sahihi ya Lugha hasa Lugha ya Taifa ya Kiswahili.


“Kwa hivi sasa rasimu ya awali imeandaliwa na tunaendela kupokea maoni kutoka kwa wadau na kuyachambua” Alisistiza Mhe. Anastazia.


Ameeleza kuwa Sera ya Lugha itasaidia  Lugha za Asilia, Lugha za alama , maandishi ya nukta nundu na Lugha za kigeni kuwekewa mkakati wa kuzishughulikia na kuzitumia kwa kukidhi mahitaji ya maendeleo endelevu ya Taifa.


Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Shani kitogo ameeleza kuwa mchakato wa kupokea maoni unaendelea na amewaomba wadau wa Lugha hasa Lugha yetu adhimu ya Kiswahili kuendelea kutoa maoni yao kwa ajili ya kupata Sera ya Lugha iliyo bora na itakayosaidia katika maendeleo na ukuaji wa Lugha nchini.


“Niwaombe wadau wa Lugha nchini waendelee kuleta maoni yao kwetu ili kuweze kufanikisha kupata Sera ya Lugha kwa Maendeleo ya Taifa Letu” Alisisitiza Bibi Shani.


Aidha Mwenyekiti wa Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Bw. Byatato Awadh ameishukuru Serikali ya waamu ya Tano kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wadau wa Lugha kwa kuanza kuandaa Sera ya Lugha itakayoleta maendeleo katika ukuaji wa Lugha nchini.


“ Niishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa sikivu kwa wananchi na wadau wa maendeleo na tunaahidi kutoa ushirikiano katika uandaaji wa Sera hii ya Lugha”Alisisitiza Bw Byabato.0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa