Na: Frank Shija – MAELEZO
FEMINA Hip yatoa tuzo tano za mwaka kwa Klabu za Fema ambazo zimefanya vizuri katika Nyanja mbalimbali.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la
Femina Hip Dkt. Minou Fuglesang wakati wa Kongamano la mwaka la Vijana
leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
huyo amesema kuwa tuzo hizo zinatolewa ili kutia chachu kwa vijana
kuongeza bidi katika kutatua changamoto zao kwa kujiamnini huku wakiwa
na ujuzi mwepesi utakaowaomgezea umakini katika shughuli zao.
“Tmezigawa tuzo hizi katika makundi makuu matano ambayo ni Mtandao Bora wa Klabu ya Fema ambayo imekwenda kwa Mwanza Federation Fema Clubs, Mshindi wa Pili wa Mtandao Bora wa Klabu za Fema iliyochukuliwa na Dodoma Students and Teachers”.Alisema Fuhlesang.
Tuzo
zingine kuwa ni Mhamasishaji Bora wa Mtandao wa Klabu za Fema wa mwaka
iliyokwenda kwa Mwalimu Christopher Mavunde, Mhamasishaji Bora wa Klabu
za Fema wa mwaka iliyochukuliwa na Mwalimu Bryson Paul kutoka Ngweli
FEMA Klabu – Shule ya Sekondari Ngweli wilayani Sengerema pamoja na
Klabu bora ya FEMA kwa mwaka ambayo ni Kisihigh Fema Club kutoka Shule
ya Sekondari Kisimiri mkoani Arusha.
Akizungumza
katika mkutano huo Mkurugenzi huyo amesema kuwa FEMINA Hip imekuwa
ikiendesha program za kuwakutanisha vijana ili kuwajengea uwezo katika
Nyanja za mabalimabali ikiwemo uongozi kwa manufaa ya sasa na baadae.
Ujuzi
ambapo vijana wamekuwa wakipatiwa kutoka kwa wataalamu wa Shirika hilo
ni pamoja na mawasiliano,mabadiliko ya mitazamo,elimu juu ya afya ya
uzazi, malezi na makuzi pamoja na stadi za maisha.
Kwa upande wake mshindi wa tuzo Mhamasishaji
Bora wa Klabu za Fema wa mwaka 2017 Mwalimu Bryson Paul amesema kuwa
Klabu za FEMA zimekuwa msingi imara wa kuwajengea uwezo wa kujitambua
vijana wengi nchini hivyo ni vyema watanzania wakatambua umuhimu wa
vijana wao kushiriki katika vikundi hivyo ambavyo vimekuwa na lengo la
kuwajengea uwezo kwa kuwapa elimu na ujuzi mbalimbali ikiwemo stadi za
maisha.
Aliongeza
kuwa binafsi amefarijika kwa kuibuka kuwa mshindi katika kipengele
hicho na kusisitiza kuwa siri pekee ni nidhamu na moyo wa kujifunza
Zaidi kwa kushirikiana na wenzako.
FEMINA
Hip imewakutanisha vijana walikatika Klabu za FEMA kutoka pande zote za
nchi katika Kongamono lililofanyika katika hoteli ya Belinda Jijini Dar
es Salaam, ambalo pamoja na utoaji wa tuzo pia vijana walipata fursa ya
kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu elimu na masuala mtambuka kwa
vijana.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment