Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » POLISI YAAGIZA MAKAMANDA WAKE KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA

POLISI YAAGIZA MAKAMANDA WAKE KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Advera-John-Bulimba-–-Kamishina-Msaidizi-wa-Polisi-ACP
Katika kuhakikisha kuwa biashara haramu ya dawa za kulevya inakomeshwa hapa nchini na kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya, Jeshi la Polisi nchini limetoa maelekezo kwa  Makamanda wa Polisi katika mikoa yote kuongeza nguvu za Oparesheni katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya kwa kuwakamata wanaotumia, wanaouza na wanaosafirisha.
Aidha, Jeshi la Polisi nchini limewaagiza Makamanda wote pindi wanapoendesha oparesheni dhidi ya dawa za kulevya kutokuangalia sura ya mtu, cheo, wadhifa wala nafasi aliyonayo katika jamii.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi nchini linakemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi wanaokusanyika katika vituo vya Polisi pindi baadhi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali wanapotakiwa kufika kwenye vituo hivyo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma wanazokabiliwa nazo. Ni marufuku kwa mtu ama kikundi chochote kukusanyika katika kituo cha Polisi bila ya kuwa na sababu ya msingi na watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Jeshi la Polisi nchini, linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu zikiwemo za watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na taarifa hizo zitafanyiwa kazi kwa siri ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa katika hali ya usalama.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-ACP,
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
MAKAO MAKUU YA POLISI.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa