Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Washiriki
watatu wa Tamasha la Majimaji Selebuka lililofanyika mkoani Ruvuma
wanatarajia kushiriki mashindano ya Mbio za Baiskeli nchini Afrika
Kusini Februari 19, 2017.
Hayo
yamebainishwa leo na Muandaaji Mkuu wa Majimaji Selebuka Reinafrida
Rwezaura wakati wa makabidhiano ya tiketi za ndege za kwenda Afrika
Kusini kwa washindi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari –
MAEELEZO jijini Dar es Salaam.
“Kikubwa
kilichotukutanisha hapa leo ni kuwaaga washindi wa Mbio za Baiskeli
katika tamasha la Majimaji Selebuka 2016, zilizofanyika tarehe 04 Juni
2016 kutoka Mbinga hadi Songea umbali wa kilomita 100, ambao wanatakiwa
kwenda kushiriki mashindano ya Mbio za Baiskeli Jijini, Johanesburg,
Afrika Kusini,” alifafanua Rwezaura.
Rwezaura
aliwataja washindi hao wanaotegemea kwenda Afrika Kusini kuwa ni Salum
Miraji ambaye alikuwa mshindi wa kwanza , Allen Nyanginywa ambaye alikuwa mshindi wa pili na Ipyana Mbogela ambaye alikuwa mshindi wa tatu.
Kwa
upande wake, mshiriki wa mashindano hayo Allen Nyanginywa ameishukuru
Taasisi ya Songea Mississippi (SO-MI) kwa kuandaa mashindano hayo pamoja
na kutimiza ahadi ya kuwasafirisha washindi wa kwanza hadi wa tatu
kwenda nchini Afrika Kusini.
Aliendelea
kwa kusema kuwa watahakikisha wanachukua ushindi nchini Afrika Kusini
kwani huko wanaenda kufanya kazi na wamefanya mashindano hayo ya
Baiskeli imekuwa ni kazi yao.
Majimaji
Selebuka ni tamasha linalofanyika kila mwaka mjini Songea, mkoani
Ruvuma ambalo huandaliwa na Taasisi ya Songea Mississippi (SO-Mi) ambapo kwa mwaka huu 2017 tamasha hilo linatarajia kufanyika kunzia Julai 23 hadi 30, 2017.
0 comments:
Post a Comment