Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Asasi
ya Marafiki wa Watoto wenye Saratani Tanzania wameandaa huduma ya
upimaji wa saratani ya watoto bila malipo itakayotolewa Februari 18
mwaka huu katika viwanja vya Donbosco vilivyopo Upanga, Jijini Dar es
Salaam.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje –
Marafiki wa Watoto wenye Saratani Tanzania, Janeth Manoni alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utoaji wa elimu juu ya kansa
ya watoto.
Bi.
Janeth amesema kuwa saratani ya watoto ni janga kubwa ambalo wananchi
wengi hawalifahamu kama linaathiri kwa kiasi kikubwa hivyo lengo la
Asasi hiyo ni kutoa elimu juu ya ugonjwa huo.
”Utafiti
uliofanywa mwaka 2015/2016 umeonyesha kuwa Tanzania tunategemea kuwa na
watu 40,000 ambao watakutwa na saratani kwa kila mwaka ambapo kati yao
watoto ni 2500 hivyo, janga hili ni kubwa kwa watoto na linahitaji
kupewa kipaumbele ili kupunguza idadi yake”,alisema Bi. Janeth.
Ameongeza
kuwa saratani za watoto zikigundulika mapema zina uwezo wa kupona kwa
asilimia 80 lakini tatizo lilopo ni kucheleweshwa kufikishwa hospitali
kwa sababu wazazi wengi hawafahamu dalili za awali za kansa hiyo.
Kwa
upande wake Muasisi wa Asasi ya Saratani Tanzania Franklin Mtei,
amesema kuwa wanaharakati wa sekta ya afya wamejitolea kutoa elimu juu
ya dalili za saratani ya watoto kupitia mitandao ya kijamii pamoja na
kutoa elimu siku hiyo ya upimaji.
Ametoa
wito kwa wananchi kujitokeza siku hiyo na kujijengea utamaduni wa
kupima afya mara kwa mara pamoja na kufanya mazoezi ili kuepuka kupata
magonjwa mengine yasiyoambukiza.
0 comments:
Post a Comment