Na Immaculate Makilika, MAELEZO, Dar es salaam
Gavana
wa Jimbo Katanga Jean Claude Kazembe amesema kuwa ili urahishaji wa
ujenzi wa daraja katika mto Lwapula uliopo katika mpaka wa Zambia na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) utasaidia kurahisha usafirishaji
wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es salaam kwenda Jimbo la Hault Katanga
DRC.
Gavana
huyo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na
waandishi wa habari juu ya ziara yake katika Badari ya Dar es salaam.
Alisema kuwa endapo nchi za Zambia na DRC zitakubaliana kujenga Daraja hilo, kutaimarisha biashara pamoja na kukuza uchumi wa nchi za Tanzania, DRC na Zambia kwa kuwa itachukua muda mfupi kwa Wasafirishaji wa Mizigo kutoka Dar es salaam kwenda DRC.
“Kujengwa kwa daraja hilo kutarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka nchini Tanzania kwenda nchini DRC, na hivyo kufanya gharama za usafirishaji wa mizigo kupungua” alisema Gavana Kazembe.
Gavana Kazembe aliongeza kuwa daraja hilo litakalogharimu dola milioni 85 litakalikuwa na urefu wa mita 700 linatarajiwa kujengwa kwa ushiririkiano wa Serikali za nchi za Tanzania, Kongo na Zambia kwa vile litanufaisha nchi hizo kiuchumi.
Aidha,
Gavana Kazembe alisema kuwa atajitahidi kushauri Serikali hizo zijenge
daraja katika mto Lwapula ili kusaidia Bandari ya Dar es salaam
kuendelea kutoa huduma nzuri za usafirishaji wa mizigo kati ya Dar es Salaam na Kongo.
Aidha,
alisema kuwa katika mazungumzo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alifurahishwa na hatua hiyo kwa kuwa itasaidia kukuza urafiki uliopo baina ya Tanzania na Kongo pamoja na kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kwa gharama nafuu.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment