Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akifungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali
za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa
Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Bandari ya Tanga.
Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam,
Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini
pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali
na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW).
Pamoja na mambo mengine, Mawaziri, Maafisa na
Wataalam wa pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba rasimu ya
makubaliano rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari
katika kipindi cha wiki mbili ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda
kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi
huo wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani
mkoani Tanga, Tanzania.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment