Na Lorietha Laurence.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa wito
kwa wadau wa michezo nchini kushirikiana na Serikali kwa kupeleka
michezo mbalimbali ikiwemo soka kwenye mashindano ya Olimpiki
yanayotarajiwa kufanyika mjini Tokyo Japan mwaka 2020 ili kupata nafasi
ya kushinda.
Ameyasema
hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na wadau wa soka katika
muendelezo wa kipindi chake cha “Wadau Tuzungumze” lengo ikiwa ni
kujadili namna ambavyo timu ya mpira wa miguu itakavyoweza kushiriki
katika mashindano hayo ya Kimataifa.
Ameongeza
kwa kusema kuwa ushiriki wa timu za mpira wa miguu kwenye mashindano
ya Olimpiki ni muhimu katika kukuza na kuendeleza soka huku akiwataka
wadau hao kupeleka michezo mingi zaidi ili kupata nafasi ya kushinda
medali mbalimbali.
“
Lengo letu ni kupata ushindi hivyo kwa kupeleka michezo mingi katika
mashindano haya ya Olimpiki tunajitengenezea nafasi nzuri ya kurudi na
ushindi na kuondokana na dhana ya kuwa washiriki ” alisema Mhe.Nape
Aidha
aliwataka watanzania kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha
tunapata ushindi kwa kuwapa moyo wachezaji wetu ikiwemo uhamasishaji
kupitia wadau mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kisasa.
“Ushindi
ni wetu sote hivyo ni wajibu wetu kuweka juhudi za dhati katika
kuhamasisha wachezaji kwa kuwapa moyo ili waweze kurudi na ushindi na
tayari nimeunda timu ya watu kumi kwa ajili ya kuhamasisha ushiriki wa
Serengeti Boys katika mashindano ya AFCON Gabon” alisema Waziri Nape.
kamati
hiyo itakayoongozwa na Charles Hillary itakuwa na wajumbe wengine
ambao ni Selestine Mwesigwa,Beatrice Singano,Hassan Abbas, Ruge
Mutahaba,Hoyce Temu,Eric Shigongo, Maulid Kitenge, Naseeb Abdul(Diamond)
na Ally Kiba.
CAPTIONS.
Na Shamim Nyaki – WHUSM
Dar es Salaam.
28 /02/2017.
PIX
1 A,B: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses
Nnauye akizungumza na wadau wa soka leo Jijini Dar es Salaam kuhusu
namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na kushinda
michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao cha Wadau Tuzungumze
kilichoandaliwa na Wizara.
PIX
2: Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Prof.Elisante Ole Gabriel akieleza jambo kwa wadau wa Soka (hawapo
pichani) kuhusu namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki
na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 leo Jijini Dar es
Salaam katika kikao cha Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara.
PIX
3: Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Omary Singo akitoa maelezo kuhusu
mikakati ya Wizara katika kufanikisha timu ya soka ya Tanzania
kushiriki Olimpiki Tokyo 2020 leo Jijini Dar es Salaam katika kikao cha
Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara.
Pix
4: Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Bw. Alfred Lukas
akichanhia mada wakati wa kikao cha kujadili namna gani timu ya Soka ya
Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo
2020 katika kikao cha Wadau Tuzungumze kilichofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
Pix
5a,b,c : Mjumbe wa Kamati ya Usuluhishi na Nidhamu kutoka Baraza la
Michezo la Taifa Bibi: Zainab Mbiro akitoa maoni yake kuhusu namna
gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo
ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao cha Wadau Tuzungumze
kilichoandaliwa na Wizara leo Jijini Dar es Salaam.
Pix
6: Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa soka
nchini baada ya kumaliza kikao cha kujadili namna gani timu ya Soka ya
Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo ya Olimpiki Tokyo 2020
kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment