Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WAZIRI NAPE NNAUYE ATEUA KAMATI YA HAMASA KUELEKEA USHIRIKI WA SERENGETI BOYS KATIKA MASHINDANO YA AFCON GABON 2017.

WAZIRI NAPE NNAUYE ATEUA KAMATI YA HAMASA KUELEKEA USHIRIKI WA SERENGETI BOYS KATIKA MASHINDANO YA AFCON GABON 2017.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameteua Kamati Maalum ya Hamasa kuelekea Mashindano ya AFCON chini ya umri wa miaka 17 yatakayofanyika mwezi May 2017 nchini Gabon ambapo Tanzania inawakilishwa na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya  Vijana (Serengeti Boys).

Kamati hiyo yenye jumla ya wajumbe nane itaongozwa na Mwenyekiti Charles Hillary kutoka Azam Tv na Katibu wake Selestine Mwesigwa ambaye pia ni katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wajumbe wa kamati hiyo ni Dkt Hassan Abass Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ruge Mutahaba Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group, Hoyce Temu Mrembo wa Tanzania mwaka 1999, Maulid Kitenge Mtangazaji kutoka EFM, Beatrice Singano Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Erick Shigongo Mkurugenzi wa Global Publishers na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba na Naseeb Abdul (Diamond Platinumz). 

Imetolewa na
SIGNATURE-ZAWADI
Zawadi Msalla       
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
28/02/2017

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa