Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma, amewataka mawakili kuangalia kufanya kazi kwa kuangalia sheria za nchi na za kimataifa

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma, amewataka mawakili kuangalia kufanya kazi kwa kuangalia sheria za nchi na za kimataifa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NA   LIDYA CHURI  - MAHAKAMA YA TANZANIA
29.06.2017
Kaimu Jaji Mkuu  wa  Tanzania,  Mhe. Profesa Ibrahim  Juma, amewataka  mawakili  kuangalia  kufanya kazi kwa kuangalia sheria za nchi  na za kimataifa ili kuweza kuwasaidia  Watanzania katika   masuala  yanayohusu sheria  hususan  wananchi wanyonge ili nchi ya Tanzania  iweze kufikia malengo ya kimaendeleo .
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Jaji Mkuu huyo, wakati hafla fupi ya  kuwapokea na mawakili wapya 248 walioapishwa na kukubaliwa kuwa mawakili, iliyofanyika leo  kwenye Kiwanja cha Mahakama  Kuu kilichopo jijini Dar es Salaam.
“Leo tumewaapisha mawakili  waliokubaliwa, nilifanya  nao mazungumzo kila mmoja, wengi wao ni vijana wadogo wenye miaka  25 hadi 30  ya  kufanya kazi ya sheria. Hivyo  kukubaliwa kwao  sio mwisho wa kusoma wanapaswa  kusoma  sheria za kimataifa ili kufahamu  sheria za utaratibu wan chi zingine,”
 Profesa Juma aliwataka  mawakili hao, hao waendelee kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia maadili  na kuepuka kujiingiza katika vitendo vya rushwa,kwa sababu     bado wananchi  wana   hisia  kwamba  tatizo la rushwa  ni kubwa  ndani ya Mahakama  ya Tanzania.
“Wazazi na Serikali imetumia  gharama  kubwa  kuwasomesha,  hivyo watambue watambue mchango huu,  waisaidie  serikali  na wazazi wao ili  Tanzania  isonge mbele, alisisitiza Lidya Churi.
 Akijibu  swali lililoulizwa na  baadhi ya waandishi kuhusu kuwepo kwa tetezi kwamba  Chama cha Wanasheria  Tanganyika(TLS),  alisema sheria  ikitungwa haitalenga  mtu wala taasisi, hivyo  hofu hiyo haina sababu  kuwepo  kwa kuwa mawakili ni sehemu ya mahakama.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa