UWASA WAPONGEZA JITIHADA ZA JPM KATIKA SEKTA YA MISITU
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
29, Juni, 2017
Umoja
wa Wavunaji Sao Hill (UWASA) pamoja na Wadau wa mazao ya miti
wamepongeza jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Pombe Magufuli za ugawaji wa malighafi za misitu kwa wenye viwanda vya
mbao.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa UWASA,
Christian Ahia pamoja na wadau wa mazao ya miti wamesema kuwa hatua
hiyo itawasaidia katika kuboresha na kupanua soko la mbao hapa nchini.
“Tunaipongeza serikali
kwa hatua nzuri iliyofikia ambapo imetoa vibali 421 kwa wawekezaji wa
viwanda vya kuchakata mbao huko Mafindi mkoani Iringa, ukilinganisha
na vibali 1,000 vilivyokuwa vimetolewa awali kwa watu ambao hawakuwa
na wawekezaji halali wa mbao” alisema Ahia.
Naye,
Katibu Mkuu wa UWASA, Dkt. Bazil Tweve alisema kuwa, serikali ina
misitu zaidi ya 15 nchi nzima, ambapo msitu wa Sao hill unazalisha
asilimia 95 ya mbao zote zinazotumika nchini, hali ambayo ilisababisha
uhaba wa malighafi katika viwanda vya kuchakata mbao kwa vile baadhi ya
wavunaji hawakuwa na sifa na vigezo vya kufanya shughuli hiyo.
“Serikali
ilifanya upembuzi yakinifu na kutoa vibali 421 kwa viwanda vya
kuchakata mbao, tunaishukuru serikali na kuipongeza kwa hatua hii muhimu
ya kuona tija ya viwanda na sisi tunaahidi kufanya shughuli zetu kwa
kufuata taratibu na sheria zilizowekwa alisema Dkt Tweve.
Hapo
awali kabla ya upembuzi yakinifu wa kubaini wawekezaji halali wa
kuchakata mbao, kulikuwa na uhaba wa malighafi ambao ulisababishwa na
utaratibu usiofaa wa ugawaji wa malighafi hizo.
Licha
ya pongezi hizo kwa serikali UWASA imesema inakabiliwa na changamoto za
masoko ya mbao zinazochakatwa nchini, na hivyo wameiomba serikali
kuwasaidia kutafuta soko ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuuza bidha
zao.
Aidha,
changamoto nyingine inayowakabili UWASA ni kiwango kikubwa cha kodi
zinazotozwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) pamoja na Halmashauri ambapo
wameziomba Mamlaka husika kuwapunguzia kiwango cha kulipa tozo hizo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment