Mratibu wa Usalama wa Dawa za Uzazi wa Mpango Kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Cosmas Swai aliyasema
hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia kuhusu matumizi ya
dawa hizo na umuhimu wake katika kupanga idadi ya watoto watakaozaliwa.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani
(UNFPA) linaadhimisha siku hiyo kesho katika Viwanja vya Mwembeyanga
ambapo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk Hamis Kigwangala atakuwa mgeni rasmi.
Alisema matumizi sahihi ya dawa hizo yanaweza kuzuia hata magonjwa
mbalimbali ya uzazi ikiwemo saratani ya shingo ya uzazi na kwamba kila
anayetumia dawa hizo na kuona kuna dalili ambazo hazifurahii afike
katika kituo chochote cha afya ili kupewa ushauri zaidi. Alisema katika
kipindi cha mwaka jana Serikali imetumia juma ya dola za Kimarekani
milioni 19 kununua dawa za uzazi wa mpango.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment