Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » KESI YA YERICKO NYERERE KUSIKILIZWA AGOSTI 22

KESI YA YERICKO NYERERE KUSIKILIZWA AGOSTI 22

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Agosti 22 mwaka huu itaanza kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili mfanyabiashara na kada wa Chadema, Yericko Nyerere.
Kesi hiyo ilipaswa kuanza kusikilizwa leo kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, imeshindikana kutokana na wakili wa Serikali anayewakilisha Jamhuri kutowepo hivyo kuahirishwa hadi Agosti 22.
Yeriko amefika mahakamani hapo bila kuwa na wakili wake, lakini upande wa Jamhuri umewakilishwa na wakili Adolfu Nkini badala ya wakili Eliasi Athanasi ambaye hakuweza kufika kutokana na kupata ajali.
Wakili Nkini alimuomba hakimu Mwijage kuahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyingine kutokana na wakili mhusika kuwa amepata ajali hivyo hataweza kufika na hakimu Mwijage aliridhia ombi hilo na kuiahirisha.
Katika kesi hiyo, Yericko ambaye anatetewa na mawakili, Tundu Lissu na Peter Kibatala, anakabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa Facebook.
Kwa mujibu wa kesi hiyo namba 184,2017, Yericko anadaiwa kufanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya mtandao namba 14 ya 2015. Na upande wa mashtaka unatarajiwa kuwaita mashahidi saba pamoja na vielelezo vingine.
Tayari Yericko alishasomewa maelezo ya awali (PH) na upelelezi umekamilika.

Chanzo Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa