Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Diwani Kata ya Sinza Mhe. Godfrey Chikandamwali akipanda mti katika Shule ya Msingi Mapambano Sinza jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mandela (Mandela day) inayoadhimishwa Julai 18 kila mwaka duniani. Zoezi hilo limeratibiwa na Mpango wa Viongozi Vijana wa Kiafrika(YALI) ikiwa ni moja ya shughuli za mpango huo. |
Diwani wa Sinza Mhe. Godfrey Chikandamwali (katikati waliokaa)akiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mapambano Bwana Abdallah Ndalakaa(kushoto kwake) pamoja na wazazi na wanachama wa Mpango wa Viongozi Vijana wa Kiafrika (YALI). Kwenye maadhimisho ya siku ya Mandela (Mandela day) inayoadhimishwa Julai 18 kila mwaka duniani. YALI waliratibu Mpango huo kwa kupanda miti katika Shule ya Msingi Mapambano Sinza jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Mpango wa Viongozi Vijana wa Kiafrika (YALI). Wakishirikiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano kupanda mti katika maeneo ya shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mandela (Mandela day) inayoadhimishwa Julai 18 kila mwaka duniani. YALI imesimamia zoezi hilo ikiwa ni moja ya shughuli za Mpango huo.
KATIKA
kuadhimisha siku ya kuzaliwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini,
Marehemu Nelson Mandela, vijana kutoka Mpango wa Viongozi Vijana wa
Afrika (YALI), wamepanda miti 50 katika Shule ya Msingi Mapambano,
Wilaya ya Kinondoni, jijini hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana diwani wa Kata ya Sinza, Bwana Geoffrey
Chikanamwali, amesifu kitendo cha vijana hao kuwa ni cha kuigwa na
kuongeza kuwa dunia sasa inahitaji miti zaidi ili kupambana na
mabadiliko ya tabianchi.
Amekihimiza
kikundi hicho kupanda miti zaidi katika maeneo mengine ya nchi ili
kuleta mabadiliko kama alivyofanya Mzee Mandela ambaye jana walitambua
mchango wake.
“Leo
tumechagua eneo la shule lakini nashauri mpande miti ndani na nje ya
Dar es Salaam ili kupambana na hali ya hewa ya ukaa inayoharibu dunia
yetu,” alishauri Bw. Chikanamwali.
Mwalimu
Mkuu Abdallah Ndalakaa amesema shule hiyo imewakilisha shule nyingine
za Tanzania katika tukio hilo na kusema vitendo vya kizalendo vilisishwe
kwa vizazi vijavyo. Marehemu Mandela na viongozi wengine wa Afrika
walipambana na ukoloni na udhalimu kwa sababu ya uzalendo, amesema.
Mandela alifungwa na makaburu kwa miaka 26.
Mwakilisha
wa YALI, Bibi Wingila Mpamila anayesoma Shahada ya Sayansi ya Afya ya
Mazingira katika Chuo Kikuu cha Muhimbili, amesema wamechagua kupand
miti kwani ni kipindi ambacho dunia inapambana na mabadiliko ya
kimazingira.
“Watu
wanakata miti hovyo, tumeamua kutumia siku hii ili kuonyesha mfano kwa
vijana wengine duniani kuokoa mazingira. Tumejitoa kama alivyojitoa Mzee
Mandela kutoka moyoni bila kutegemea malipo,” alisema Bi. Mpamila.
Julai 18, ni siku ya kuzaliwa Nelson Madiba Mandela na uazimishwa na watu wanaothamini mchango wake.
0 comments:
Post a Comment