Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mfanyabiashara
Yusufali Manji (41) bado anaumwa na amepelekwa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Hayo
yameelezwa leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, mbele
ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi yake na wenzake watatu
ilipotajwa.
Katuga
aliiambia mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika na akaomba kesi
hiyo ipangiwe tarehe nyingine. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 4,
2017.
Katika
kesi hiyo, Manji na wenzake wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya
sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa
vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya
zaidi ya Sh 200 milioni pamoja na mihuri.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Deogratius Kisinda(28), Abdallah Sangey(46) na Thobias Fwere (43).
Awali,
akiwasomea hati ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao, Wakili wa
Serikali, Tulumanywa Majigo amedai kuwa Juni 30,2017 katika eneo la
Chang’ombe ‘A’wilaya ya Temeke Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja
wamekutwa na askari polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa
vinavyotumika kushonea sare za Jeshi la Wananchi Tanzania zenye thamani
ya Sh 192.5milioni na kwamba mali hiyo ilipatikana kinyume cha sheria.
Katika
shtaka la pili, Wakili Majigo alidai kuwa Julai Mosi, 2017 huko
Chang’ombe ‘A’ washtakiwa hao walikutwa na polisi wakiwa na mabunda
manane ya vitambaa vinavyotumika kushonea sare za Jeshi la Wananchi
Tanzania zenye thamani ya Sh44 milioni mali ambayo ilipatikana isivyo
halali.
Katika
shtaka la tatu, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Juni 30, 2017
Chang’ombe ‘A’ walikutwa na muhuri wa Jeshi la Wananchi Tanzania wenye
maandishi ‘Mkuu 121 kikosi cha JWTZ’ bila ya kuwa na uhalali kitendo
ambacho kingehatarisha usalama wa nchi.
Wakili
Majigo katika shitaka la nne, anadai kuwa Juni 30, 2017 kwenye eneo
hilo la Chang’ombe ‘A’ Manji na wenzake hao watatu walikutwa wakiwa na
muhuri wenye maandishi’ Kamanda Kikosi 834 KJ Makutupola Dodoma bila ya
kuwa na uhalali kitendo ambacho kingehatarisha usalama wa nchi.
Shitaka
la tano, Manji na wenzake hao wanadaiwa kuwa Juni 30, 2017 huko
Chang’ombe ‘A’wamekutwa na muhuri wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania wenye
maandishi (Commanding Officer 835 KJ Mgambo P.0. Box 224 Korogwe)
kitendo ambacho kingehatarisha usalama wa nchi.
Katika
shtaka la sita, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Julai Mosi,
2017 katika eneo hilo la Chang’ombe ‘A’ walikutwa na askari polisi
wakiwa na namba za usajili SU 383 ambayo ilipatikana kwa njia isiyo
halali.
Kwenye
shtaka la saba washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Julai Mosi, 2017 kwenye
eneo hilo la Chang’ombe ‘A’ washtakiwa hao walikutwa na skari polisi
wakiwa na namba za usajili wa gari SM 8573 ambayo ilipatikana kwa njia
isiyo halali.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote
kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza
kesi hiyo.
Manji na wenzake wanatetewa na mawakili Hudson Ndusyepo, Malimi Seni na Emmanuel Safari.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment