Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » NMB KUSHAURI BIASHARA ZA FEDHA

NMB KUSHAURI BIASHARA ZA FEDHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker

KATIKA kutekeleza sera ya viwanda nchini, Benki ya NMB ambayo inashirikiana na mitandao ya benki za kimataifa zaidi ya 30, wametangaza huduma mpya ya kutoa ushauri na kusaidia wateja katika biashara za kifedha.
Huduma hiyo ijulikanayo kama Trade Finance, itawezesha kampuni au watu binafsi kufanya manunuzi ya vifaa kutoka nje ya nchi na usafirishaji wa bidhaa kutoka ndani ya nchi kwa kutumia makandarasi ambao watatoa uhakika wa kufanya shughuli hizo.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema benki hiyo pia inachukua jukumu la ubadilishaji wa nyaraka dhidi ya malipo.

Alisema huduma hiyo iliyoanzishwa mwaka 2012 na benki hiyo, inawajibika moja kwa moja kuhakikisha malipo baada kutekeleza mkataba, kusimamia mnunuzi na muuzaji au mkandarasi na mtoa kazi ili kuhakikisha uaminifu baina yao.
Bussemaker alisema pia NMB inaweza kukopesha muingizaji na msafirishaji au muagizaji na msambazaji wa bidhaa katika biashara za kimataifa ndani ya nchi.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Trade Finance, Linda Teggisa alitaja nyaraka muhimu ambazo mteja anatakiwa kuwa nazo ni ankara, orodha ya mizigo iliyofungwa, hati ya mizigo melini, hati ya mizigo angani, hati ya uasilia wa bidhaa, nyaraka nyingine za usafirishaji na bima.

Alitaja pia aina ya dhamana ambazo wanatoa ni ya zabuni ambayo ni ya kumsaidia mkandarasi anayeomba zabuni za mikataba ya kazi ambayo kwa kawaida ni asilimia tano.

Chanzo Nipashe

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa