Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI

SERIKALI KUUNDA KAMATI YA KUKAGUA VIWANDA VYOTE NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo.
Wanahabari wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameunda kamati itakayo shirikisha wakuu wa mikoa yote Tanzania,  kwa Viwanda vyote vilivyobinafsishwa kuvitembelea na kuvikagua na kutoa taarifa ya maamuzi kwa viwanda vitakavyokuwa havifanyi kazi kwa kutokutii agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mkoani Pwani katika ziara yake ya kutembelea na kuzindua viwanda.
Waziri Mwijage ameyasema hayo leo ofisini kwake alipo kukutana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ambapo alisema adhma ya serikali ni kuhakikisha viwanda vinalindwa na kuongeza uzalishaji lakini pia serikali imejikita zaidi katika kuwasaidia wananchi kupata ajira katika viwanda.
Aliongeza kuwa, wengi walipenda kuanzisha viwanda kwa bei rahisi sana lakini wameshindwa kuviendeleza na wengine kufanya shughuli tofauti na iliyokusudiwa, Waziri amesema kamati hii itakaa Dar es salaam ambapo itashirikisha wataalamu kutoka idara mbalimbali za serikali na kupitia Viwanda vyote ili kuvikagua na kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi.

Pamoja na hilo la ubinafsishaji, Mwijage amezungumzia swala la Mchele wa bandia ambapo taarifa zimekuwa zikizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Tanzania tunazalisha mchele bandia,  na kusema kuwa Tanzania hakuna mchele bandia na taarifa hizi ambazo zimekuwa zikisambaa zinaharibu jina la nchi yetu kwani sisi ni wazalishaji na wasambaji wakubwa wa mchele kwa nchini mbalimbali.

Waziri ameahidi kufanya ufuatiliaji muda wote na atakapopatiwa taarifa zozote kuhusiana na upatikanaji wa mchele bandia kwa kuomba kupigiwa simu kupitia no. 0800110827.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa