Na.Agness Moshi-MAELEZO
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imekua mkombozi kwa wagonjwa wa moyo
Afrika Mashariki kufuatia kupungua kwa gharama za matibabu ukilinganisha
na ilivyokua hapo awali.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mbunge wa jimbo la
Dokolo nchini Uganda Bi.Cecilia Barbara alipotembelea taasisi hiyo ili
kuona na kujifunza jinsi Serikali ya Tanzania inavyotoa huduma za Afya
kwa wananchi wake .
Bi.Cecilia
amesema taasisi hii ni msaada mkubwa kwa Afrika Mashariki kwasababu
itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa moyo wanaopelekwa nchini India
au Afrika Kusini kwa matibabu kama ilivyo awali baadala yake
watatibiwa Tanzania au nchini kwao.
“Tunahitaji
kubadilishana mawazo kama wana Afrika Mashariki, kwasababu kwa kuja
hapa tumegundua tunavifaa na uwezo wa kupunguza gharama za matibabu ya
moyo“ Alisema Bi.Cecilia.
Bi
Cecilia amesema kutokana na ubora huduma zinazotolewa na taasisi hii
tangu kuanzishwa kwake serikali ya Uganda imekubali kuja kutembelea
Tanzania ili kujifunza na kuanzisha mradi kama huu.
“Hatukujua
kama Tanzania kuna mradi mkubwa kama huu na unaofanya kazi nzuri lakini
kwa kuja tumejua na tunategemea kuanzisha mradi kama huu japo
itatuchukua muda kufikia hatua iliyofikiwa na Tanzania”aliongeza
Bi.Cecilia .
Naye
Afisa Mwandamizi Kitengo cha Utafiti wa Bunge la Uganda Mhe. Jonathan
Enamu amesema kuwa amejifunza mengi kwenye ziara hii na ameona ni jinsi
gani gharama za matibabu zimepungua kwa wagonjwa wa moyo. “Nimejifunza
mengi, ikiwemo jinsi ya kupunguza gharama za matibabu na namna bima za
afya zinavyoweza kutumika katika matibabu“ alisema Bw. Enamu.
Naye
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi
amesema kuwa , wanatoa huduma kwa watu wote kuanzia daraja la chini na
watu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uganda,comoro,Yemen na Kenya.
Prof.Janabi
amesema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kutumia shilingi bilioni 1.65
badala ya shilingi bilioni 4.72 ambayo ni sawa na kupunguza takribani
asilimia 65 ya gharama za matibabu ya magonjwa ya moyo nchini kama
wangewapeleka India kwa matibabu
Prof.
Janabi alifafanua kuwa kwa mgonjwa mmoja wa maradhi ya moyo anatibiwa
kwa shilingi milioni 35-40 tofauti na nchini India ambapo mgonjwa mmoja
anatumia shilingi milioni 120.
Aidha
Profesa Janabi ameishukuru Serikali kwa kuipa ushirikiano taasisi hiyo
kwani kwa mwaka huu wa fedha Taasisi imepokea asilimia 100 ya bajeti
itakayosaidia kuendesha shughuli zao kwa kiwango cha kuridhisha.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Mbunge wa ilala Mhe. Azzan Mussa Zungu (MB)
amesema kuwa wamewapeleka wageni hao kwenye taasisi ya moyo ili
waweze kujifunza na kuona ni jinsi gani Tanzania imefanikiwa kupunguza
gharama za matibabu kwa wagonjwa wa moyo
“wameona
namna sisi Tanzania tulivyopunguza gharama kutoka kuwapeleka watu 300
kwa mwaka nje kwa matibabu ya moyo mpaka sasa watu wanne tu, ambao
tunawapeleka si kwa sababu hatuna uwezo bali ni kwa sababu ya vifaa
havijakidhi “ alisema Mhe.Zungu.
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete ilianzishwa rasmi mwaka 2014 inashughulika na
utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wa moyo, kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa
udaktari,ufamasia na uuguzi. Pia taasisi hii inashirikiana na nchi
nyingine duniani kwa kubadilishana maarifa,uzoefu na kufanya mafunzo
mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment