Na: Paschal Dotto - MAELEZO
Kampuni ya “Kuja Na Kushoka Tools Manufactures Group”
imeunga mkono jitihada za serikali utunzaji mazingiza na kuwa na uchumi
wa kati kupitia viwanda kwa kubuni mashine inayotengeneza nishati ya
mkaa mbadala kwa kutumia mabaki ya mazao na takataka badala ya kukata
miti.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dare es salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Leonard Kushoka amesema kuwa ugunduzi huo utarahisisha matumizi ya nishati hiyo ambayo ni mkombozi kwa wananchi wa kipato cha kati na chini.
“Teknolojia
hii ni njia mbadala na salama kwa mazingira kwani inatumia taka za aina
zote pamoja na mabaki ya mazao badala ya kukata miti, vilevile ni njia
ya utunzaji wa mazingira kutokana na takataka hizo kutumika katika
kuzalisha mkaa kwa matumizi ya nyumbani”. Alisema Kushoka.
Bw.
Kushoka ameongeza kuwa katika miji mikubwa kama Dar es salam, Mwanza
na Arusha matumizi ya nishati ya mkaa ni makubwa kutokana na kuwa na
idadi kubwa ya watu ikiwa jiji la Dar es salam pekee matumizi ya mkaa
yanafikia magunia 28,000 kwa siku sawa na asilimia 50 ya mkaa wote
unaozalishwa nchini ikifuatiwa na Mwanza na Arusha.
Aidha
Bw.Kushoka alisema kuwa mashine hiyo yenye uwezo wa kuzalisha magunia
20 ya mkaa kwa siku inatumia nishati ya mafuta ya dizeli au umeme
kutegemea na matakwa ya mteja na inauzwa kwa shilingi milioni 15.
Bw.
Kushoka aliongeza kuwa licha ya mashine hiyo kulinda mazingira pia
inaongeza thamani ya mazao kwani mabaki yote ya mazao yanatumiwa na
mashine hiyo kuzalishia mkaa mbadala kama malighafi.
0 comments:
Post a Comment